Kuwa Pro Russia au Pro US, kigezo huwa nini?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Kuna watu hakuna Jema la Russia duniani kama ilivyo watu wengine wanaoamini Marekani haina Jema hata Moja hufanya duniani.

Sasa kwa watanzania wenzangu, huwa mnatumia kigezo gani kuamua kuwa upande wa Marekani au wa Russia. Huwa mnazingatia mambo gani hasa?
 
Beberu US Anauma na kupuliza Beberu Russia Anang'ata kama mamba akiuma anapiga na lock..
Jambo jingine ni hili!;
Russia alimuuzia Ndege vita iddi Amini!
Sisi alituuzia ant aircraft missile!
Tulipo ishiwa mabomu ya heat seeking missile's!; mrussi alikataa kutuuzia mabomu Hadi Kwa Hard cash au Mikataba migumu Kwa dhamana ya Mali Asili!
Huku Ndege vita za iddi Amini zinatamba Hadi Mwanza Visiwa vya Saa nane!
Lengo lake lilikuwa vita yetu na Uganda iwe Endelevu Ili auze silaha zake!
Kukosa Hekima ya J.K.Nyerere Kuomba msaada wa hayo mabomu Msumbiji na Algeria!; Ile vita ingekuwa ni simulizi
Ukiona Mtu anaishabikia Russia ujue miaka hiyo alikuwa yupo kiunoni au mtoto au Ashki majunun...
nyingine!😇😭
Hiyo Ilinikera Hadi Sasa kuichukia Russia....
 
Ni kama tu kuwa shabiki wa Simba au Yanga. Hakuna kigezo.
 
Kwa uzoefu wangu mdogo nadhani mambo hizi dini tumelewa na majahazi inachangia pakubwa mtu kushabikia upande upi

Wakristo wengi sana wapo upande wa USA na washirika wake NATO pamoja na Israel na WISLAM wengi sana wapo against na USA kwa madhila anayoyasababisha mashariki ya kati kitovu cha uisla, hivyo basi waislam wanalazimika kushabikia hasimu wake mkubwa ambaye ni Russia na washirika wake Iran korea na China

USA amekua na mvurugano sana na mashariki ya kati ambapo kuna Waislam wengi na hivyo waislam kuchukulia kwamba USA inauhasana na uislam huku ikiwatetea na kuwapandelea Waisrael
 
Hapo ni mambo matatu.
1. Mifumo ya kisiasa.
Ni mara chache sana ukutane na mfuasi wa ujamaa asiipende Urusi and vice versa.
2. Masuala ya dini.
Muislamu auto tu kwenye maongezi ataonyesha haipendi USA ila moyoni mwake anajua mwenyewe and vice versa
3. Chaguzi bila vigezo kama ilivyo soka.
Mwisho kuna wale mashabiki tu, hawa nchi zinawachagua kama ilivyo vilabu vya mpira, anajikuta tu ni mpenzi wa hiyo nchi.
 
Akili timamu tu.
Wanaoshabikia USA wanaunafiki, chuki au ulimbukeni. Na ndio hao hap pro israel.

Mtu anashabikia Israel akipewa msaada na USA kuua wapalestina akidhani Israel ndio ukiristo, kisha Israel hiyo hiyo yampa siraha Azabaijani kuua wakristo wa Armenia just because Armenia iko close na Russia.

Ni mjinga ndie anaedhan Israel ana give a fac about christianity.

Nimeikataa propaganda ya West tangu sijui internet nasikiliza BBC kijijini huko. I have never being deceived by those two face monsters.
 
Mi binafsi ni kwa vile baba alisoma Urusi,na alirudi na sare za jeshi na makoti Urusi.

Vyombo vya jikoni vina miaka 35 bado vinatumika,haviishi chuma chuma na alminium alminium.
sasa hawa ndio walimu wa baba yangu ntaacha kuwapenda.Sema mji walio patia shule ni Ukraune wakati huo ipo Russia.
 
Ni Kuchagua Unachokiamini mkuu kiwe na maana lakini.Binafsi Role Model wangu ni Putin The Bear.
 
Uwezo wa kusoma na kuchambua background details na analytical thinking ukifa kinachobakia ni hulka ya ushabiki usiojali mantiki. Ni tatizo la elimu na uelewa.

Sina Kiswahili sahihi cha maneno niliyowekea italics.

Kwa kifupi, kuwa pro hiki au pro kile katika mambo halisi (factual) ni ufinyu wa akili - au kujipa burdani dhanifu tu.
 
Kuna watu hakuna Jema la Russia duniani kama ilivyo watu wengine wanaoamini Marekani haina Jema hata Moja hufanya duniani.

Sasa kwa watanzania wenzangu, huwa mnatumia kigezo gani kuamua kuwa upande wa Marekani au wa Russia. Huwa mnazingatia mambo gani hasa?
Kwa 90% Kuwa Pro US
Lazima Uwe na uwezo mdogo Kichwani yaani Unameza Propaganda Kuliko Uhalisia
Pili unakuwa na Akili za Kitumwa Kuamin US ndio kila kitu kwenye hii Dunia
Yaani unaamini kila wakifanyacho US nisahihi na Hawana Makosa yeyote.
Kuwa Pro US Huna Uwezo wa Kujiuliza Kile kilicho Tangazwa na Vyombo vyote vya West hususan BBC , VoA, Fox NBC, CNN nk yaani Kila Habari itakayo tolewa na Hawa Unaimeza Mazima Mazima huna muda Wa Kujiuliza .
 
Kwa upande wangu nimekuwa nikakuta USA anafanya ubabe Ulio wa wazi wazi Kwa mataifa Ambayo USA Anataka Rasilimali zao anavamia hizo nchi na kufanya unyama uliopitiliza ana waacha watu wataifa Hilo wakiwa vilema wengine wakiwa mayatima na Hiyo nchi inabaki kuwa masikini wa kutupwa Huku Miji ya nchi husika ikibaki kuwa magofu so Hiyo ni sababu moja wapo ilyojifanya niwachukie USA
 
Beberu US Anauma na kupuliza Beberu Russia Anang'ata kama mamba akiuma anapiga na lock..
Jambo jingine ni hili!;
Russia alimuuzia Ndege vita iddi Amini!
Sisi alituuzia ant aircraft missile!
Tulipo ishiwa mabomu ya heat seeking missile's!; mrussi alikataa kutuuzia mabomu Hadi Kwa Hard cash au Mikataba migumu Kwa dhamana ya Mali Asili!
Huku Ndege vita za iddi Amini zinatamba Hadi Mwanza Visiwa vya Saa nane!
Lengo lake lilikuwa vita yetu na Uganda iwe Endelevu Ili auze silaha zake!
Kukosa Hekima ya J.K.Nyerere Kuomba msaada wa hayo mabomu Msumbiji na Algeria!; Ile vita ingekuwa ni simulizi
Ukiona Mtu anaishabikia Russia ujue miaka hiyo alikuwa yupo kiunoni au mtoto au Ashki majunun...
nyingine!😇😭
Hiyo Ilinikera Hadi Sasa kuichukia Russia....
Mashabiki wa Urusi wana vinasaba na mashabiki wa kubwa la magaidi duniani yaani Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
 
Kwa upande wangu nimekuwa nikakuta USA anafanya ubabe Ulio wa wazi wazi Kwa mataifa Ambayo USA Anataka Rasilimali zao anavamia hizo nchi na kufanya unyama uliopitiliza ana waacha watu wataifa Hilo wakiwa vilema wengine wakiwa mayatima na Hiyo nchi inabaki kuwa masikini wa kutupwa Huku Miji ya nchi husika ikibaki kuwa magofu so Hiyo ni sababu moja wapo ilyojifanya niwachukie USA
Mfano?
 
Kwa uzoefu wangu mdogo nadhani mambo hizi dini tumelewa na majahazi inachangia pakubwa mtu kushabikia upande upi

Wakristo wengi sana wapo upande wa USA na washirika wake NATO pamoja na Israel na WISLAM wengi sana wapo against na USA kwa madhila anayoyasababisha mashariki ya kati kitovu cha uisla, hivyo basi waislam wanalazimika kushabikia hasimu wake mkubwa ambaye ni Russia na washirika wake Iran korea na China

USA amekua na mvurugano sana na mashariki ya kati ambapo kuna Waislam wengi na hivyo waislam kuchukulia kwamba USA inauhasana na uislam huku ikiwatetea na kuwapandelea WaisraelNi kwe

Kwa uzoefu wangu mdogo nadhani mambo hizi dini tumelewa na majahazi inachangia pakubwa mtu kushabikia upande upi

Wakristo wengi sana wapo upande wa USA na washirika wake NATO pamoja na Israel na WISLAM wengi sana wapo against na USA kwa madhila anayoyasababisha mashariki ya kati kitovu cha uisla, hivyo basi waislam wanalazimika kushabikia hasimu wake mkubwa ambaye ni Russia na washirika wake Iran korea na China

USA amekua na mvurugano sana na mashariki ya kati ambapo kuna Waislam wengi na hivyo waislam kuchukulia kwamba USA inauhasana na uislam huku ikiwatetea na kuwapandelea Waisrael
Kwa hiyo Waislam wa Nzega wanawachukia pia waislam wa Marekani? Halafu wanawapenda Hezbollah na Hamas na Urusi. Hahaha
 
Kwa 90% Kuwa Pro US
Lazima Uwe na uwezo mdogo Kichwani yaani Unameza Propaganda Kuliko Uhalisia
Pili unakuwa na Akili za Kitumwa Kuamin US ndio kila kitu kwenye hii Dunia
Yaani unaamini kila wakifanyacho US nisahihi na Hawana Makosa yeyote.
Kuwa Pro US Huna Uwezo wa Kujiuliza Kile kilicho Tangazwa na Vyombo vyote vya West hususan BBC , VoA, Fox NBC, CNN nk yaani Kila Habari itakayo tolewa na Hawa Unaimeza Mazima Mazima huna muda Wa Kujiuliza .
Kwa hiyo bora kuwa Pro Russia?
 
Kuna watu hakuna Jema la Russia duniani kama ilivyo watu wengine wanaoamini Marekani haina Jema hata Moja hufanya duniani.

Sasa kwa watanzania wenzangu, huwa mnatumia kigezo gani kuamua kuwa upande wa Marekani au wa Russia. Huwa mnazingatia mambo gani hasa?
Kigezo ni uwe na uwezo wa kuisaliti nchi yako kwa maslahi ya hao wakubwa.

Watu badala ya kuwa Pro Tanzania, wapo bize na nchi zilizojengwa na raia wao kwa jasho na damu. Tunashobokea sana visivyo vyetu wakati tuna akili kama wao.

Tanzania damned country
 
Back
Top Bottom