Kuwa tajiri kwa mtaji wa laki 3 tu kupitia ufugaji wa kuku wa kienyeji

Jaribuni. Mimi nilijaribu kutoka mwaka juzi. Nimejifunza mengi. Kati ya mambo niliyojifunza ni kuwa veterianry officers ambao si wafugaji ni wababaishaji tu. Ushauri wao siyo reliable sana. Afadhali mfugaji mwenyewe akikupa ushauri unasaidia sana.
Nikweli mkuu! Yaan Kuna Mambo unaweza kumuuliza Kama ushauri yeye analeta za vyuoni! Pia wanakejeri na dharau, mfano Mimi Kuna mmoja nilimwambia naomba ushauri nataka nifuge kuku kuanzia 100 eti akaniuliza " na huo ni ufugaji?" Nikamwambia ndio! Akasema kila la kheri!

Chaajabu nikamkuta hum anatafuta ajira kwa wafugaji wa kuku!
 
Mfano tu yeye mara ya mwisho kula kuku wa kienyeji lini.

But inawezekana ukiweka nia. Masoko yapo.
 
soma maoni ya ndugu chipolopolo kuku wanachangamoto za magonjwa ambayo kiuhalisia hata ukiwauliza wataalam wenyewe hawana majibu,kwa ushaur ni bora upige stoo ya ngombe uutakutoaa ila uwe mvuumili,ufugaji wa ngombe na kuhakikishia ndani ya miaka 5 we ni milionea
 
Ni fursa nzuri mkuu tatizo ni mahali...yani sehemu ya kuwafugia hao kuku....kwa upande wangu hyo laki 3 pengine na zaidi ninayo lakini sehemu ya kufugia ndo tatizo..........
Upo wap mkuu?
 

Hadithi Nzuri. Inavutia. Ikiwa katika giza nene la utekelezaji wake wa muda mufupi. Itabidi usubiri miaka mingi sana kufika hapo ulipokusudia
 
Sio kweli Kuna MTU anafuga ngombe mwaka wa kumi huu ila maisha ni mgumu anaganga njaa tu
 
asante sana mkuu nami nitaanza kwa majike 5 tu majogoo mengi kwa majirani
 
.
 
Mkuu are You serious kuku wa kienyeji 11 ndani ya miezi 3 utakuwa na kuku 300+ ???

Uongo sio kitu kizuri kabisa.... Nataka nifanye utafiti kwa kukutembelea najua utakuwa na record ya kuku wa kuanzia 11 then tuone hadi sasa una kuku wangapi????
Kweli kaibisa ni kitu ambacho hakiwezekani. Kwanza kuna siku 21 za kulalia, kuna siku saba za kupoteza wakati anaanza kuumba mayai, kuna vifaranga baadhi kufa kutoka na hali ya hewa
 
Noted japo si rahisi hivyo
 
umenena ukweli mtupu
Nimeanza mwezi March na kuku 35 tu
Leo ninao kuku 120 (110 ni vifaranga na mayai tunaokota karibu 5 kila siku)
Ninaona taa ya kijani mbele maana soko ni uhakika kabisa
Hivi kina uwezekano mtu mwenye kuku 60 akafikisha kuku 3500 Kwa miaka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…