Kuwa tajiri kwa mtaji wa laki 3 tu kupitia ufugaji wa kuku wa kienyeji

Aiseee iko poa sana hiii
 
ninauza kuku wa kienyeji wakubwa majogoo kwa mitetea wanaoanza kutaga.njoo inbox.
 
Ila gharama za kutengeneza banda ni kubwa mno japokuwa itakuwa tofauti kulingana na eneo. Kwa ujumla inawezekana kabisa kama Maelezo yalivyo. Kumbuka ukifaulu kupambana na changamoto ndio mafanikio hayo.
 
Hapa dawa ni kufanya kwa vitendo...maana story za ufugaji ni nyingi Sana...wengine wanasema inawezekana wengine wanapinga...kuhusu soko kwa dar Sina Shaka...maana huwa naona magari makubwa yakipita yamepakia kuku wa kienyeji kutoka mikoani karibu Kila siku.
 
Banda ni simple,nunua yale mabox yanakuja na pikipiki,kama sikosei huuzwa 5000 kwa moja,matano tu yanatosha na bati kama tatu za kuezekea,wiremesh kwa ajili ya madirisha ,
ili kuku wa kienyeji watage tofauti na wakijijini ni chakula tu chenye virutubisho,
magonjwa ni chanjo na dawa,hawa wanaokufa baada ya chanjo basi dawa itakuwa inakuwa fake,
kuku wa kisasa ni delicate sana,lakini kuna makampuni makubwa yanafuga kuku kwa maelfu,tena wanabanana kwenye cage kama wafungwa mda wote na hawatoki kuzurura lakini hawafi kivile na ni biashara ya mamilioni
 
Unaweza kuweka sample ya picha ya hizo box zilivyo? Na zinauzwa wapi?
 
yanapatikana kwa wauzaji wakubwa wa pikipiki ,ukienda maduka yanayouza pikipiki ulizia,kuna mtu hapo juu kama sikosei kaweka picha ya vifaranga kwenye box,mabox kama hayo
 
Hiv kuku wa kienyej unaweza uka wafuga kwa Ku wafungia ndan kama hawa kuku wa kizungu" maana Nina vyumba viwili dabo vipo tupu
Sio kuwafungia kwa nje unaweza uzio wawe watoka na kuingia kuku wa kiswaz ukimfungia hta kukua inakua ngumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…