Kuwa tajiri kwa mtaji wa laki 3 tu kupitia ufugaji wa kuku wa kienyeji

Aksante kwa madini haya yamenihamsha akili
 
Maboresho kidogo ya uzi,
1. (Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300) si kuku 10 bali ni kuku 11 hivyo ni gramu 1430 kwa chakula chetu kitatupeleka tabribani siku 95.

2. (Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240) wastani wa hutagaji kwa kuku wa kienyeji nahisi kuna shida sina uhakika na utagaji wa zaidi ya siku 15, naomba ufafanuzi kwa hili? Matarajio yangu ni mayai 120-180 kwa mwezi.
 
Mtoa mada nakuunga mkono!! Kuna fursa kwenye kwenye ufugaji pamoja na kwamba mambo yanaweza yasiende sawa kama ulivyoandika maana haujaconsider risk
 
>Kuku wa kienyeji kufika uzito wa kuweza kuuzwa ni miezi 8 hadi 12.

>Kuku wa kienyeji uwa hatagi kila siku na ni wachache sana wanaweza taga hata mayai 20 katika mzunguko mmoja.

>Kuku wa kienyeji uwa anapumzika kutoka mzunguko mmoja wa kutaga hadi mwingine.

>Utunzaji wa vifaranga bila kutumia mama kuku una gharama mf chanzo cha joto, madawa, chanjo.

>Kuku wa kienyeji hata akiwa anakula chakula cha kuku wa kisasa ukuwaji wake ni ule ule kulingana na mfumo wake wa vinasaba

>Ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara una changamoto nyingi sana ndio maana ni kazi sana kumkuta mtu mwenye kundi la kuku hata mia tatu wa kienyeji.

>Ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara una changamoto sana ndio maana miradi yote ya kufanya ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara lazima uje na mpango wa kuboresha ufugaji kwa kuingiza kuku chotara. Mfano RLDC na RIU

Taarifa:
Mwaka wa 8 huu nipo ktk ufugaji wa kuku, hakuna changamoto ambayo sijakutana nayo na sijafika hata robo ya ndoto yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa Iringa utamuuzia nani kuku 18000?
 
be
i ya jumla ni 8000 braza
Yaani kilimo bwana ndo hapo kinapokuwaga kitamu. Wewe ushahangaika ukapiga hesabu ila mnunuzi akija anakupangia bei. Mbona kwenye nyanya mwaka jana wanunuzi walichemka, mpaka yule jamaa wa Iringa akavuna milioni 400 ndani ya mwezi mmoja!
 
Ila we jamaa ni muongo au hujawahi fuga kuku wa kienyeji.
Yani kuku kumi tu kwa siku uokote mayai nane 🙄. Mi nafuga kuku zaidi ya Mia wa kienyeji na sijawahi okota mayai 50 toka nimeanza kufuga mwaka 2014.
Nyie ndo huwa mnafanya watu wanaingia wanatupangia Bei za kununua mayai or kuku kwa kudhani tunavuna Sana kumbe wenzetu mnafugia kwenye madaftari🤔🤔🤔
 
Hii michanganuo kwa kuisoma hivi tu inaonekana ni simple ila ukienda field sasa.
mi ni mfugaji,asee inaitaji moyo sana kufuga ila ukiwezea inalipa kweli lkn muda na userious sana inaitajika sio rahisi na pia ni rahisi inatemea na wewe
 
Huu unaitwa ufugaji wa kwenye Daftari, haunaga hasara kabisa, Pia kilimo cha kwenye daftari hasa cha mapapai na matikiti kinalipa kinoma.
Ukija kwenye uhalisia ni very hatarious
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…