Kuwa tajiri kwa mtaji wa laki 3 tu kupitia ufugaji wa kuku wa kienyeji

Its a nice idea sema inahitaji kujitoa kweli na kuwa na uvumilivu mixer subira
 
Haya mambo yakifanyika kwa uzuri naona umasikini unavyokimbia Tanzania
 
Iko vzur apo ni mtaji. Tuh. But. Magonjwa ya kuku nayo ni tatizo aysee
 
Ufugaji wa Excel na Kilimo cha Kutumia M-Pesa kimeumiza wengi sana
 
Hamna banda la sh 60,000 labda ukate miti na fimbo porini ndio utapata,juu uezeke na majani ya miti utayoyakata Ila hayo mabati ya reject hata ulikute lina kutu kiasi gani Huuziwi chini ya 2000 - 3000 sasa bado mbao,misumari,usafiri,nk

Laki 3 unayoiongelea ukipigia hesabu ya KUKU TU kidogo nakuelewa ila sio kuanzia banda hadi kuku wenyewe na chakula Juuu Hapana hapo unaingiza watu kwenye majuto mkuu.

Sijaona mahali umeweka gharama za DAWA za hao kuku,maana kwa kuku wote hao kuwapa dawa na dawa zenyewe ndio zipo kwenye vichupa vidogo na zinauzwa BEI hapana sikubaliani la hilo.

Kwa mradi huo tena wa kuwaachia kuku wazurure wenyewe ni kumtakia mtu anaeanza kufuga HASARA sio kila mtu ana endeo la kuachia kuku hivyo,wezi hawapo hivi eeh? magonjwaaa?? tena kuku wazururaji ndio kabsaaa sio wakutegemea kibiashara.

Kidogo ungeshauri watu wafungie kuku ndani na kuwajengea eneo la kuzurura ambalo mtu utaweza li control ila sio kufunglia kuku wakazurure,Hapo ni kumsababisha mwenye ki LAKI 3 chake akipoteze bureeee AJE kulaani BIASHARA ambayo ni nzuri kumbe tatzo ni mwalimu kalisha wanafunzi matango PORI.

banda ulilosema lijengwe kwa gharama uliyotaja ni banda la kufugia NJIWA AU sili au Sungura sio KUKU tena kuku wa biashara.HAPANA.
 
Ni rahisi sana kwa kusoma nenda shule yake sasa

Uvumilivu na kujituma ni mhimu sana.
 
Mbona vinapatikana vyote ?
Ona hii Incubator ya mayai SABA.
haifiki hata 100,000/=

Nataka hiyo incubator, ntaipataje??
 
Nimekuelewa vzr sn mkuu
 
Ni idea sahihi na ina ukweli unaowezekana ndani yake...

Binaafsi pia ni mfugaji... Alichosahau ni suala la magonjwa na urahisi wa kufa kwa mifugo.... Izo kinga alizozisem mazee zinatibu kibahat bahat unaweza ukawapa na ukakuta woote wamekufa asubuh.....

Alafu karahisisha saaana..... Lazima upambane sio simple kama unavyosoma.


Changamoto ya kuku ni hapo tu..... Kwingine koote hakuna tatizo kabiisa. Na inawezkan...
 
Tatizo kubwa hapa watu wengi wamezoea kupinga kila kitu! naomba niwambie kitu kimoja.
Kija jambo unaloliona lilianzia kwenye wazo. Hata binadamu alianzia kwenye neno (biblia inatuambia hivyo)
Hata wewe unayesoma hapo ulianzia kwenye neno toka kwa baba yako kwenda kwa mama yako, walipokubaliana ndo wakatenda - mimba ikapatikana ... mama akalea mimba .. miezi 9 ukafunguka!
Acheni kupinga kila kitu - tenda!
 
Watu wanapinga pinga saana. sijui wao wanafanya shughuli gan ambayo haina hasara wala changamoto
 
Watu wanapinga pinga saana. sijui wao wanafanya shughuli gan ambayo haina hasara wala changamoto
Ni roho za kishetani ...
Mimi niliwahi kununua vifaranga chotara 100, wakafa sana wakabaki vifaranga nane (8) tu na kati ya hao walikuwepo majogoo 2. Sipaswi kutoa ushuhuda huo kwa wengine kwa sababu nilijua kosa langu ...
Baada ya hapo nilinunua tena vifaranga 200; wife alichukia sana akisema naharibu hela ... hawa 200 walikua 187 hadi kuanza kutaga .. majike walikuwa 145, majogoo 42; huyo huyo aliyechukia (wife) ndo alikuwa wa kwanza kunishawishi atafute wateja wa kuyanunua hayo majogoo na kunishauli nitoe jogoo mmoja nimpeleke kanisani kama shukrani ya pekee.
Namaanisha nini?
Wapinzani wa maendeleo / mafanikio yetu sio mitandaoni tu; wengine tuko nao majumbani.
Ushauri, usisite kuthubutu!
 
Safii mkuu, vp mradi mpaka sasa umefikisha kuku wangap
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…