Kuwa tajiri kwa mtaji wa laki 3 tu kupitia ufugaji wa kuku wa kienyeji

Jamani ni kweli kupeana ujuzi wa kuwa wajasiliamali. Kwa kifupi nianze hivi.
tunapo taka kufanya jambo haijarishi lina faida ndogo au kubwa lazima kwanza tuishirikishe mioyo yetu. Waweza pewa detail za kutosha jinsi ya kuanza mradi wa kuku na faida ikawa kubwa kwa kusoma makaratasi au makara mbalimbali. Hivyo unavyo soma au unavyo ambiwa sivyo ilivyo kwako au itakavyo kuwa kwako. Wewe itakuwa tofauti. Na kama hujawahi kufuga hata kuku mmoja ukamtunza usilaumu hayo makaratasi au maneno. Wanao paswa kutumia hayo makaratasi ni waliothubutu kwa kiasi fulani na sasa wanapanda nngazi. Si kwa wewe unaye fikiri iwe hivyo.
aksanteni nitarudi kwa somo dogo.
 
ufugaji wa kuku hasa kienyeji.kiuhalisia haikupi faida haraka,chukulia kama unahifadh fedha yako baada ya muda utapata faida.AU ni kama umenunua hisa,baada ya muda fulan utapata mgao. Kuku faida yake ni baada ya miezi 5 - 6, hapo ndo unaeza ona matunda ya kile ulichopanda kwa miez 6. Nadhan ndio katika ufugaj invist ya mda mfupi.
 
Ni fursa nzuri mkuu tatizo ni mahali...yani sehemu ya kuwafugia hao kuku....kwa upande wangu hyo laki 3 pengine na zaidi ninayo lakini sehemu ya kufugia ndo tatizo..........
Pole mkuu
 
Mkuu miguu 50×50 ni sawa na mita ngapi kwa ngapi?
 
Mkuu are You serious kuku wa kienyeji 11 ndani ya miezi 3 utakuwa na kuku 300+ ???

Uongo sio kitu kizuri kabisa.... Nataka nifanye utafiti kwa kukutembelea najua utakuwa na record ya kuku wa kuanzia 11 then tuone hadi sasa una kuku wangapi????
nadhani anachofanya kuwawekea mayai 15 and probly watatotoa 14hadi 12 inategemea hali ya hewa mm nimefanya na naendelea kufanya huwa wanatoto hadi 14 ,then unawaacha na mama zao kwa wiki 3 watarudia tena kutaga baada ya wiki moja then siku 21 ya kutaatamia
 
msada zaidi hapa,umesema mayai ya kwenda kutotolesha yasikae zaidi ya siku 12?
 
mkuu usisahahu kuwa kila zama na kitabu chake.
 
msada zaidi hapa,umesema mayai ya kwenda kutotolesha yasikae zaidi ya siku 12?
Yana kuwa bora zaidi yasipo zidisha siku 9 tangu kutagwa kutokana na utunzaji... Ila mpaka siku 12 yanatotoleka kwa probability ndogo. Yakizidi hapo yanaleta shida
 
Mkuu ukifuga kisayansi hiyo hesabu itafika. Tatizo lako wewe unafuga kwa mazoea.
 
Jaribuni. Mimi nilijaribu kutoka mwaka juzi. Nimejifunza mengi. Kati ya mambo niliyojifunza ni kuwa veterianry officers ambao si wafugaji ni wababaishaji tu. Ushauri wao siyo reliable sana. Afadhali mfugaji mwenyewe akikupa ushauri unasaidia sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…