Uchaguzi 2020 Kuwagawa Watanzania kwa misingi ya kodi si vizuri

Uchaguzi 2020 Kuwagawa Watanzania kwa misingi ya kodi si vizuri

sammosses

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Posts
1,687
Reaction score
1,111
Kampeni za Uchaguzi mkuu kwa madiwani, Wabunge na Urais unaendelea nchini, kwa kila chama kunadi sera Zake kutafuta kuamininiwa na wenye mamlaka ya kutoa madaraka kwa serikali kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Mengi tumesikia kutoka vyama vyote, lakini lipo moja kubwa lisipo tazamwa kwa umakini mkubwa tunaliingiza Taifa kwenye misingi ya ubaguzi.

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano ,utekelezaji wa sera kwa serikali itakayopewa ridhaa na wananchi kuwaongoza utachagizwa na ukusanyaji kodi,utakaofanywa na serikali kwa mujibu wa sheria.

Na shughuli zote za kujiletea maendeleo baada ya ukusanyaji kodi utapangiwa bajeti na serikali kwa idhini ya bunge la Jamhuri ya Muungano ambacho ndicho chombo cha uwakilishi wa wananchi.

Na kodi inayo kusanywa na taasisi ya mapato iliyo idhinishwa na bunge itakusanya mapato hayo kwa mujibu wa sheria bila ubaguzi kwa wananchi wake.

Halikadhalika bajeti kuu ya serikali inayo letwa bungeni na serikali na kuidhinishwa na bunge itatekelezwa kwa misingi ya haki na usawa kwa wananchi bila ubaguzi.

Na kwa kuzingatia kuwa, nchini yetu ipo chini ya mfumo wa vyama vingi, ukiukwaji wowote wa sheria utakaofanywa kwa misingi ya ubaguzi wa matumizi ya kodi hiyo, itakuwa kinyume na utaratibu wa sheria na kuvunja umoja wa kitaifa kwa misingi ya ubaguzi.

Yanayo tokea sasa katika kampeni zinazo endelea mbali na kuto kukemewa na taasisi zinazo simamia uchaguzi, zinapaswa kukemewa kwa ukali na wadau wa kodi(wananchi) wanao tozwa kodi bila ubaguzi, lakini wakibaguliwa katika matumizi ya kodi hiyo, kwa msingi wa hawa Wapinzani sisi chama tawala!!!!

Rais wa Jamhuri ya Muungano ni rais wa Tanzania kwa mujibu wa sheria japo atapatikana kupitia mgongo wa vyama vya siasa, halikadhalika wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano ni wawakilishi wa wananchi bila kujali mwamvuli wa vyama walivyopitia.

Anapotokea rais aliyeko madarakani au mgombea wa urais akataka kuwagawa Watanzania kwa misingi ya kiitikadi za kivyama anapaswa kupingwa na kuogopwa kama ukoma, huyo hakubaliki asilani abadani!!!!

Tumeona na kumsikia mgombea urais wa CCM akiwabeza wananchi wa majimbo ya uchaguzi walio chagua/watakao wachagua wabunge wa vyama vingine mbali na chama anachotoka yeye, serikali yake haitapeleka maendeleo iwapo atachaguliwa kuwa rais wa nchi hii.

Kauli hii mbali na kutolewa mara kwa mara kabla ya kampeni na baada ya kampeni, imewashtua sana walipa kodi wa nchi hii kwa kuwabagua na kuikanyaga ibara ya 8 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano kuwa msingi mkuu wa serikali baada ya kuipa serikali madaraka ni ubaguzi katika kusimamia ustawi wa wananchi,kwa kuwagawa kwa itikadi zao.

Bahati mbaya sana kauli hii ya kibaguzi mbali na kuleta athari kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita imegeuzwa utamaduni unaokwenda kuzoeleka.

Ni vizuri kama imeshindikana kumkemea mjivuni huyu, basi utozaji kodi nao unapaswa kutekelezwa kwa msingi ubaguzi kwa wale wanaonyimwa kupelekewa maendeleo kwa makosa ya kuwachagua wapinzani, sasa iwe mwisho kutozwa kodi kwa kuwa matumizi ya kodi hayawahusu.

Niviase vyama vyenye wagombea, waenzi misingi iliyo wekwa na Mwalimu Nyerere juu ya umoja na mshikamano wa kitaifa, kwa kukemea wagombea wao wanao wagawa Watanzania kwa itikadi za vyama vyao.

Pia ni vizuri wananchi kuwachagua viongozi watakao heshimu katiba yetu, kwa kuhifadhi na kutekekeza matakwa ya katiba hiyo na kuheshimu haki za binadamu na watakao wajibika na kutokuwatisha wananchi.

Tanzania ni nchi yetu sote,watch out!
 
Back
Top Bottom