Kuwapiga picha wanafunzi wakifanya mtihani wa Taifa kunawaathiri kisaikolojia

Kamura

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2011
Posts
507
Reaction score
52
Nimesikitishwa na kitendo cha waandishi wa habari kuingia na video camera kwenye chumba cha mtihani na kuwapiga picha wanafunzi wakati wakifanya mtihani.

Kitendo hiki kinaweza kuwaathiri kisaikolojia na kuwafanya washindwe kufanya vizuri mitihani yao ikizingatiwa kwamba wanafunzi waliopigwa picha ni wa mikoani ambao kwao tukio hilo halijazoeleka sana kwao.

Ninashauri jambo hilo lifanyike baada au kabla ya wanafunzi kufanya mitihani si wakati wa mitihani. Habari hiyo ilirushwa jana TBC1 saa 2.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…