Kuwashwa Kwa kiganja cha mkono na kucheza Kwa jicho kunakupa taarifa itakayotokea

Unaposema mara ngapi unamaanisha nini kwenye Akili yako ndogo?
Unaniuliza Mimi badala ya kujiuliza wewe mwenyewe.

Nimekuambia, kuhusu Elimu na Pesa itabidi utafute washirika wenzako ili angalau uweze kunipata.
Sasa nijiulize mimi kivipi wakati wewe ndio umesema ukiwashwa mkono unapata pesa, Na mimi nimekuliza ni mara ngapi haukuwashwa mkono na umepata pesa! Acha kuleta hadhithi za abunwasi... Fanya kazi

Kuhusu Elimu na Pesa, wewe huna Elimu... Ungekuwa na Elimu ungeanza kufanya research kwanza kabla ya kuamini Utopolo wako, kitendo cha kuamini huo utabiri tambitambi ni kuonyesha Elimu yako ni duni. Alafu pia Pesa sio matako. Pesa inaongea yenyewe, kwanza ungekuwa na pesa usingeleta mada za kidwanzi kama hizi, sisi wenye pesa hatunaga hizi kelele za kutamba mitandaoni, ungekuwa na pesa mbona unaamini kwenye utabiri tambitambi wa kuwashwa mkono na kucheza jicho. Dalili za kuwa wewe ni kapuku.
 

Pole Sana.
Watu wa Aina yako ni wakuonewa huruma tuu.
 

Hizo "reflexes" na spasm za mwilini ni uhai tu, tusivitie ushirikina.

Hujawahi kuchezwa na makalio (piriformis syndrome)? Soma kuhusu "sciatic nerves".
 
Hizo "reflexes" na spasm za mwilini ni uhai tu, tusivitie ushirikina.

Hujawahi kuchezwa na makalio (piriformis syndrome)? Soma kuhusu "sciatic nerves".

Sasa tutaenda kujadili Kwa hoja.

Hapo hakuna ushirikina wowote.

Mungu alivyoumba maumbile ya dunia na viumbe aliweka na Lugha zitakazoleta maana(mawasiliano) katika maumbile hayo au viumbe hivyo.

Uchunguzi wowote uwe wa kisayansi au kiimani/Kiroho au Nafsi utazingatia Lugha zilizopo katika maumbile au viumbe hivyo.

Hata hospitali Madaktari hupata ugonjwa au matarajio kupitia hizo Lugha(ishara, dalili, Alama, Sauti n.k.) kupitia vile utakavyomwambia au atakavyoona kwenye mwili wa mtu au kiumbe.

Kufafanua Lugha, au maumbile au Viungo vya mwili sio ushirikina.
Ni kama Kwa wana jiolojia ambao hawawezi kuichunguza miamba yote wanapotafuta Dhahabu, Bali wataangalia ishara, Alama, dalili za Dhahabu katika eneo husika.

Zipo maana za kibaolojia, kinafsi, Kiroho, kijiografia n.k

Mfano kwenye Jiografia hasa kwenye utabiri wa Hali ya hewa, kinachomfanya ni kuangalia Lugha zilizopo katika anga.

Hata kuzaliwa Kwa mitume, Watu wenye Akili hutumia hizo ishara kujua huyu ni mtume au sio.
Mfano hasa katika dini ya kiislam, Padri Walaqah yeye sio kwamba alifanya shiriki kumjua Muhammad kuwa ni mtume. Ila aliangalia signs, dalili, Alama n.k.

Hata kwenye Kiyama Watu hujui hizi ni siku za mwisho wa Dunia kupitia Dalili, ishara, Alama....

Hakuna shirki hapo.

Shirki ni kumshirikisha uwezo wa Mungu na vitu vingine au watu wengine.
Ila kuelezea mambo ya Mungu sio shirki.
 
Hizo "reflexes" na spasm za mwilini ni uhai tu, tusivitie ushirikina.

Hujawahi kuchezwa na makalio (piriformis syndrome)? Soma kuhusu "sciatic nerves".

Kwa kuongezea pia, ubongo unafanya kazi Kwa namna mbili, Kwa hiyari yako na kuna mambo ambayo huna hiyari nayo.

Nafsi ya mtu inadili zaidi na Matendo yasiyo ya hiyari kama moyo kudunda, kupepesa macho, jicho kucheza n.k.

Kufikiri, yapo mawazo ambayo unaweza amua kufikiri na yapo ambayo unashangaa tuu unafikiri, hujui Nani anaamua au anayazalisha katika ubongo wako. Yale ambayo huamui isipokuwa unajikuta tuu unafikiri mengi asili yake ni Nafsi yako.

Sasa wenye Elimu za kukariri najua watakuja Hapa.
 
Waislam tunaaiita "fitrah".
 
Uko sahihi kama Mimi nikijikwaa mguu wa kushoto ni jambo baya ila nikijikwaa kulia ni jambo zuri tena linafanyika Siku hiyohiyo
 
Utapata hela nyingi muda si mrefu, fanya kazi kwa bidii na heshimu kila unaekutana nae kazini [emoji28][emoji1787]
 
"Wanasema ukiwashwa kiganja ni dalili ya kupata pesa na vipi ukiwashwa kalio ni dalili ya nini?

NAY WA MITEGO - TRU BOY
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…