Mabobish
JF-Expert Member
- Jul 25, 2018
- 367
- 282
Mwenzenu kwa muda mrefu sasa nimekuwa na tatizo la kuwashwa sana kwenye unyayo wa miguu tena kwa kubadilika badilika miguu.
Aidha wakati mwingine nimekuwa na tatizo la kuwashwa sana kwenye kiganja cha mkononi hususani kwenye dole gumba au vidole vingine kimojawapo.
Tendo hili limekuwa likinitokea mara kwa mara katika wiki wakati mwingine huweza kunitokea mara tatu au nne kwa wiki, kibaya zaidi hutokea muda wowote si usiku si mchana, kwa wakati wa usiku naweza kuwa katikati ya usingizi mzito lakini mara tu hali ya kuwashwa inapotokea basi lazima niamke kwa kustuka usingizini.
Kinachofuata ni kujikuna kwa muda mrefu takribani dk 20 mpaka 30 tena kwa ama kutumia brush ngumu au jiwe la kuogea ndipo muwasho unaisha. Katika kujikuna sometimes mpaka eneo ninalojikuna linachubuka ndo inakuwa kupata ahueni kwangu.
Wadau naomba mwenye kufahamu hali hii inasabishwa na nini na tiba yake ni nini mnisaidie maana kibaya zaidi muwasho mkali hutokea wakati wowote hata kama nilikuwa naendesha gari basi hulazimika kupark gari, kuvua Kiatu in case imetokea unyayoni kisha kujikuna mpaka hali itulie.