SoC04 Kuwatunza na kulinda watoto dhidi ya unyanyasaji

SoC04 Kuwatunza na kulinda watoto dhidi ya unyanyasaji

Tanzania Tuitakayo competition threads

hanny088

New Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
2
Reaction score
0
Unyanyasaji kwa watoto ni tatizo ambalo la weza sababishwa na mtu mzima au mtoto kwa mtoto linalomfanya mtoto athirike. Laweza kumuathiri mtoto kimwili, kihisia, kingono. Pale tunaposhindwa kuwatimizia watoto mahitaji ya msingi hupelekea unyanyasaji kwa watoto ambalo ni tatizo linaloongezeka siku baada ya siku na sababu kuu ikiwa ni umaskini.

Watoto wadogo ndio wahanga wakubwa wa vitendo hivi vya kikatili ambavyo vimekuwa vikifanywa na watu wa karibu ikiwemo wazazi, ndugu na majirani. Sababu nyingine nyingi zinazopelekea unyanyasaji ni pamoja na kukosa Elimu ya kumlea mtoto katika maadili ya msingi na kusababisha unyanyasaji,matatizo ya kifamilia na tamaduni hatari ambazo zinaaminiwa na kupelekea unyanyasaji kwa watoto, matatizo ya kisaikolojia kwa watu wa karibu wanaoishi na watoto, msongo, pamoja na huzuni kwa watu wa karibu na watoto.

Unyanyasaji kwa watoto hupelekea mtoto kuumia, kuchubuka kimwili na matatizo ya afya ya kimwili ambayo huleta matatizo ya mda mrefu ya kihisia. Kutokana na unyanyasaji huu hupelekea mtoto kupitia changamoto ya afya ya kiakili na changamoto nyingine nyingi katika mahusiano, tabia, uaminifu na mawasiliano, huharibu maendeleo ya mtoto katika lugha, kuongea na kujifunza.

Kipi kifanyike kuweza kulinda taifa letu la kesho na kupata Tanzania tuitakayo:

Wazazi tujifunze namna ya kulea watoto kwa ukaribu:
Tutaweza kupunguza tatizo la unyanyasaji kwa kujifunza kuwa wazazi bora ilikuleta mabadiliko, tuwe karibu na watoto kwa upendo na pamoja na kanuni, kwa kula nao pamoja hatakama tukiwa na majukumu mengi ya kazi, tujitahidi kutenga mda kwaajili ya watoto wetu hii itatusaidia kujua matatizo yanayo wakumba wanapokuwa mashuleni, nyumbani na pamoja na njiani. Tusisahau kuwafundisha watoto kujua mambo ya msingi kama elimu ya kiroho, na ya kimwili ikiwemo kujitunza na kujua haki zake.

Wazazi tusikae kimya pindi tatizo linapojitokeza:
Tujifunze kupambania haki za watoto wetu kwa kufanya nafasi yetu kwa sababu wao wenyewe hawawezi kujitetea. Tuangalie kesho yetu si tu leo. Tuwe watu wanaosimama sambamba pamoja na kuwalinda watoto kwa kutoa taarifa dhidi ya unyanyasaji kwa watoto kwa madawati husika.

Serikali ijitahidi kutengeneza mfumo thabiti na mahususi wa kulinda watoto:
Pamoja na mfumo iliowekwa wa namna ya kutoa taarifa dhidi ya unyanyasaji kwa watoto, Jamii pia inahitaji kupewa elimu ya namna ya kutumia mifumo hio na wasamalia wema wahakikishiwe usalama na usiri pindi watakapo toa taarifa dhidi ya unyanyasaji wa aina yoyote unaofanyika kwa watoto na taarifa inapotolewa basi serikali ichukue hatua kwa haraka kwa kuchunguza na kupunguza milolongo ilikuweza kumlinda mtoto na kupunguza athari za zaidi.

Sera na sheria ziimarishwe kwa uthabiti:
Wote watakao bainika wakihusishwa na ukatili sheria ichukuliwe Kwa udhabiti kusiwe na nafasi yeyote ya mtu kuwa juu ya sheria kwakuwa kila mtu yupo chini ya sheria. Adhabu itakayotelewa kwa yeyote aliyehusika iendane na kosa la mshtakiwa. Hii itasaidia kupunguza na kuweza kutokomeza janga hili la ukatili kwa watoto.

Tujifunze kutokumuadhibu mtoto tukiwa na hasira:
Matukio ya unyanyasaji kwa watoto ikiwemo kimwili na kihisia ni pale tunapomuadhibu mtoto tukio na hasira, hii hupelekea kutokea kwa matukio hatarishi kama mtoto kuuguzwa moto, mafuta na matukio mengine mengi yanayomuathiri mtoto kisaikolojia na kimwili. Pale mzazi unapojiona unahasira jizuie kumuadhibu mtoto na utafute mda ambapo hasira zimepungua iliuweze kutoa adhabu stahiki.

Tupunguze na kuzuia ubinafsi kwenye famili zetu:
Wazazi wengi tunashindwa simama kwenye nafasi zetu za kuhakikisha tunawatunza watoto wetu kwa uzuri na usahihi. Hii inatokana na sisi wazazi kujiangalia wenyewe pekee,kwakuogopa kushusha hadhi ya Familia juu ya aibu inayojitokeza na kupelekea Familia kukaa kimya kiasi ya kwamba hakuna kilichotokea, kwakuogopa kuharibu ndoa na kuchukiwa ndani ya Familia.

Elimu na ufahamu itolewe kwa udhabiti kwanzia ngazi ya kata, vitongoji, mitaa ilikumgusa kila mmoja katika jamii:
Elimu thabiti itokanayo na programu za malezi katika maendeleo ya watoto wetu itakayotelewa mitaani na namna ya kuwalinda, utoaji taarifa utakapofundishwa katika jamii zetu hii itapunguza unyanyasaji kwa kiasi kikubwa kwa sababu kila mmoja atajua namna ya kumlinda mtoto kwa kujua ya kwamba mtoto anahuhitaji wa usaidizi wa karibu. Elimu hii pia iwepo mashuleni kwakuwa na programu za kuzuia unyanyasaji kwa watoto.

Tulenge uwezeshaji kiuchumi ilituweze kupunguza umaskini:
Umaskini ni changamoto kubwa inayoleta na kusababisha unyanyasaji kwa watoto. Tuhimize jamii katika mafunzo ya ufundi ya nayohusisha kutumia mikono. Katioka mafuzo haya ya ufundi itasaidia taifa kwa ujumla kwa kuongeza kipato na kupunguza unyanyasaji kwa watoto.Mafunzo ya ufundi yahamasishwe katika jamii na mashuleni.

Kwa kufanya yote haya kwa udhabiti na kwa bidii tutaimarisha malezi yetu na kulinda kesho ya watoto na kuweza kupata Tanzania tuitakayo.

p7-katuni.jpg

Kutoka kwa hisani ya mtotonews.com
 
Upvote 2
Back
Top Bottom