Kama ilivyo kwenye board za mazao kama bodi ya kahawa,bodi ya pamba,korosho n.k. Kama ilivyo kwenye majeshi kuna Jwtz,polisi magereza,uhamiaji n.k. Hata walimu tutenganishwe katika chama wale wa msingi wote na wa chekechea wawe na chama chao kiitwe kwa kimombo Tanzania Primary School Teachers Association(TPSTA). Wale wa sekondari nao wawe na chama chao ambacho kiitwe Tanzania secondary school Teachers Association(TSSTA). Hii itapunguza kusalitiana wakati wa kudai haki zetu walimu, pia itataua kero za walimu kwani kunaweza kuwa na naibu mawaziri wawili wa sekondari na msingi na waziri muhimu mmoja. Pia kunaweza kuwa na makatibu wakuu wawili wa primary na secondary. Ikitokea uozo itakuwa rahisi kujua wapi kuna uzembe. Ni mawazo yangu tu hayo yanaweza kuwa mazuri au mabaya, nawasilisha.