SoC01 Kuwe na kibao cha kuripoti uzembe ofisi zote za serikali kama ilivyo rushwa ili kuongeza ufanisi wa taasisi

SoC01 Kuwe na kibao cha kuripoti uzembe ofisi zote za serikali kama ilivyo rushwa ili kuongeza ufanisi wa taasisi

Stories of Change - 2021 Competition

buffalo44

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2016
Posts
4,678
Reaction score
11,357
Salaamu wakuu.


Taasisi za kiserikali ni muhimu sana kwenye kuchangia upatikanaji wa maendeleo kupitia utoaji huduma ambao utawezesha kufikia malengo ikiwamo kupunguza rushwa, urasmu na umasikini.

Napendekeza kuwe na kibao kila taasisi inayohudumia wananchi. Chenye namba za kuripoti kukitokea ucheleweshwaji wa huduma bila sababu za msingi, urasimu, na uzembe wowote ule.
Ili kufanya hivi serikali inatakiwa kukaa na taasisi zote na kupigia hesabu rasimali zilizopo zinaweza kutoa huduma kwa wastani wa mtu mmoja mmoja kwa muda gani? Rasimali ikiwamo wafanyakazi na vitendea kazi.
Ikifikia muafaka wa muda uwekwe kwenye kibao. Mfano.

MUDA NI NUSU SAA AU LISAA LIMOJA.

KIBAO KINASEMA.

IKIWA HUJAPATA HUDUMA ZAIDI YA SAA 1, BILA SABABU ZA KUELEWEKA PIGA 222
KURIPOTI
SERIKALI INAKUJALI.

Sababu zinazotakiwa kutolewa ni!
• Dharura ya ghafla na hiyo dharura inatakiwa kuwa na thibitisho wa mkuu wa sehemu ulipo.
• Lunch
• Muda wa kazi kuisha.
Kuundwe idara chini ya taasisi kama TAKUKURU
Itakayokuwa inapokea simu za malalamiko kila mfanyakazi anakuwa idarani pale pale.

Ukiripoti ikigundulika ni kweli hatua kali zichukuliwe ili iwe fundisho kwa wengine, kama kusimamisha kazi kuona sababu kama zina mshiko apewe onyo arudishwe ikiwa ni uzembe kweli kweli kazi iishe.

Faida ya hii ni;
Tutasaidia kuwa na taasisi zinazopiga kazi kweli kweli.
Wafanyakazi watakuwa watu wa kazi sio longo longo bila sababu.
Inaweza saidia nchi kuaminika hata kuvutia wawekezaji ambao wanaweza weka headquarters hapa nchini kutoa ajira maana mambo yanaenda fasta bila longo longo.
Itapunguza rushwa na urasimu.

La Mwisho: Nchi hii ni yetu sote kuwa na njia yetu ya kutatua matatizo yaweza kutuongezea nguvu ya kusimamia rasimali tulizonazo kuongeza ufanisi

Natumai serikali itaangalia hapa.
Nipo tayari kukosolewa.
Karibu kwa mawazo tofauti.
Uongozi wa JamiiForums naushukuru kwa fursa hii.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom