SoC04 Kuwe na mageuzi ya TAKUKURU na CAG ili kukomesha rushwa, ufisadi, ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za umma yanayoibuliwa kila mwaka na CAG

Tanzania Tuitakayo competition threads

Masha2020

New Member
Joined
Jun 20, 2024
Posts
2
Reaction score
1
Mabadiriko yanatakiwa kufanyika katika utendaji wa Takukuru na CAG ili kuzuia ubadhirifu na ufisadi katika miradi na fedha za uma zinazotolewa na serikali. Kama sheria ya 2007 inayoipa takukuru mamlaka ya kuzuia rushwa, ufisadi, ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha ya serikali.

Awali ni kurekebisha sheria za Takukuru na CAG ziwe taasisi huru na wawe na mahusiano ya karibu katika kazi zao ili waambatane. Halafu wafanye yafuatayo

1. Takukuru na CAG kuainisha miradi yote iliyopelekewa fedha na kuwa taarifa sahihi za miradi hiyo kabla ya kutekelezwa .

2. Takukuru na CAG washiriki hatua zote za mwanzo za vikao kabla ya manunuzi kufanyika au kutekeleza mradi.

3. Takukuru na CAG washiriki vikao vyote vya upatikanaji wa wazabuni wa kutekeleza miradi husika au manunuzi husika.

4. Takukuru na CAG wafuatilie na kukagua kila hatua ya utekelezaji wa miradi inapokamilika kabla ya malipo ya fedha kufanyika au manunuzi kufanyika.

5. Takukuru na CAG washughulikie mapungufu ambayo yatagundulika mapema kabla fedha haijapotea badala ya kushughulikia wahusika wakati fedha ,muda na rasilimali nyingine vimeshapotea.

6. Aidha CAG na Takukuru waboreshe miongozo ya ukaguzi wake kwa kufanya kila robo mwaka na inapobidi muda wowote badala ya kufanya kwa mwaka.

7. Kila mradi au manunuzi ya umma yanapotengewa fedha , fedha hiyo ijumuishwe na gharama za ukaguzi wa mradi huo ili kuepuka wakaguliwa kuwahonga wakaguzi.
 
Upvote 7
Chapisho Zuri lakini CAG Office haiwezi kukubali kuambatana pamoja na TAKUKURU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…