Hivi karibuni (Mwezi Juni 2024) wakati Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania, Tulia Ackson akitangaza maamuziya kumsimamisha Mbunge Luhaga Mbinakushiriki vikao 15 vya Bunge pamoja nashughuli nyingine za Kibunge alisema moja yasababu ya kufanya hivyo ni kwa kuwa Mpinaalikiuka na kudharau Kiti cha Spika.
Kabla ya kuitwa kwenye mchakato wa kesiyake hiyo Bungeni Mpina alishtakiwa kwakutoa taarifa za maelezo yake kwaWanahabari kabla ya kufanyiwa kazi naMamlaka inayohusika Bungeni.
Nimeanza na mfano huo kuonesha jinsiambavyo kunatakiwa kuwa na uwajibikajiinapotokea kuna kitu hakipo sawa hasa kamahujatimiza au umekiuka taratibu za majukumuyao (sijamaanisha Mpina alikosea, nimezungumzia taratibu tu).
Nitoe mfano wa pili, Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anaweza kuamuakutengua nafasi za wateule wake mudawowote akitaka, iwe kwa kuweka sababu au kutoweka sababu, hivyo ndivyo ilivyo hatakatika taasisi nyingine mbalimbali za kazihasa zisizo za Kiserikali.
Nimeanza na mifano hiyo ili mada au hojayangu iweze kueleweka vizuri hapa chini.
Kama Bunge linaweza kumsimamisha au kumfukuza au kumuondoa Bungenimwakilishi wa Wananchi kwa njia yoyote, hiyo inamaanisha wale waliomteua wanakosauwakilishi Bungeni, kwa nini wale wanaofanya maamuzi ya kumpa nafasi hiyoMbunge au Rais (ambao ni Wananchi) hawanamaamuzi ya kumuondoa kama hajatimiza kileambacho ametumwa na Wananchi?
Kwa miaka mingi imekuwa ni kawaida kuonaWananchi wakilalamikia Mbunge waokutokuwa ‘active’ Bungeni au wakatimwingine kutotimiza yale aliyoaahidi wakatianatafuta Ubunge iwe kwa makusudi au kwabahati mbaya lakini bado halazimiki kusemachochote au kujieleza kwa nini hajafanya kilealichoahidi.
Kwa nini hizi nafasi za kisiasa Wananchi ambao ndio hasa wanaompa nafasi hiyoMbunge au Rais hawana mamlaka yakumuondoa au kumuwajibisha mtuwaliyemteua badala yake wanalazimikakusubiri miaka mitano ambayo ataitumikiandio waje wamuwajibishe kupitia sanduku la kura?
Hatuoni kwamba kwa mifumo kama hiyoJamii au Wananchi wanaendelea kuteseka kwakuwa tu Katiba au Mifumo hayampi nafasi yakumuwajibisha Mbunge wake?
Tumeshuhudia Nchi kadhaa baadhi yaviongozi wakiondolewa madarakani kwamitutu ya Bunduki au kwa nguvu ya umma ambapo taratibu zinazotumika sio sahihi.
Hapo namaanisha kuna matumizi ya nguvu, kwa nini Tanzania tuendelee kuwapaWananchi maumivu wakati ni jambo ambalolinaweza kubadilika?
Maendeleo ya Wananchi ambayo ndio maishaya watu yanafanyiwa majaribio, kwambawanajiuliza wampe fulani labda ataweza,akipewa nafasi (Mbunge) kwa kuwa anajuaWananchi haohao waliompa kura hawawezikumuondoa mpaka wasubiri miaka mitano au 10, basi kinachofanyika ni kuwa wapole hukuwakiendelea kuumia kimyakimya.
Kuna mifano mingi ya Wabunge ambao wapondani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania, ushiriki wao ndani ya Bunge ni wakiwango cha chini, hawatoi uwakilishiunaotakiwa kwa Wananchi, imekuwa ikidaiwakuwa wanatumia nafasi hiyo kwa ajili yakuneemesha mambo yao binafsi kwa cheo cha Ubunge.
NINI KIFANYIKE?
Najua ni ngumu kupitishwa na Wabungewenyewe kwa kuwa wao ndio wanufaika nahawawezi kutunga Sheria au Kanuni ambazozinaweza kuwabana wenyewe lakini kupitiaStories of Change 2024, naomba ujumbe huuuwafikie wote wajue kuwa kama ilivyo nguvuya umma katika kumuweka Mbunge na Rais Madarakani, hivyohivyo ikiamua kumuondoainawezekana.
Badala ya kutumia nguvu kamatunavyoshuhudia katika Nchi nyingine, inatakiwa uwepo utaratibu maalumnitakaouelezea hapa chini.
Mbunge anapochaguliwa na Wananchi kwaajili ya kuwawakilisha kwa kipindi chake cha Miaka mitano, inatakiwa inapofika nusu yamuda wake, kama Wananchi waliompa nafasihiyo wanaona kabisa kuwa hafai kuendeleakuwa mwakilishi wao wanatakiwa kuwa nanafasi ya kutoa maoni, kupiga kura yakutokuwa na imani naye.
Kama Bunge linao uwezo wa kupiga kura yakutokuwa na imani na Rais, kwa niniWananchi wanakosa haki hiyo wakati waondio wamewaajiri viongozi waliopomadarakani?
Itungwe Sheria au utengenezwe utaratibu, Wananchi wawe na uwezo wa kuibua hojahiyo, kisha wakiona inafaa kuwepo nautaratibu wa kujiandikisha kupitia daftari la Mtandaoni au liwe linapatikana katikamamlaka za Jimbo na wakifikia kiwangofulani cha kujiandikisha mfano nusu yawapiga kura wa Jimbo, basi kuwe na utaratibuwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani namwakilishi wao.
Kawaida Mawaziri wanakuwa na heshimakwa Rais na Chama kilichowapa nafasi kwakuwa tu Rais ana nguvu ya kuwateua na bilachama hawawezi kuupata uwakilishi huowalionao, lakini Wabunge hawawezi kuwa nahofu hiyo kwa Wananchi wanaowatumikiahata kama wanajua wanachokifanya sio sawa.
Demokrasia inatakiwa kuoneshwa kwavitendo, Sheria au mfumo huo utaongezauwajibikaji kwa Wawakilishi wakijua kuwakama hawatatimiza ahadi zao au kuoneshamwelekeo watawajibishwa.
Kumuacha Mbunge ‘ale kuku’ miaka mitano, kisha akiondoka Wananchi wafanye majaribiokwa Mwanasiasa mwingine kwa kumpa miakamitano, maendeleo yatabaki kutegemea utashiwa kiongozi wa juu ngazi ya Rais.
Najua Wabunge wao sio kwambawakizungumza ndio maendeleo yatakuja, lakini wakitambua kuna uwajibikaji wa ainahiyo utasaidia wao wajitambue na wajue zile‘gharama’ walizotumia kuingia Bungenihazitarudi kama wataendelea kulala nakutowatumikia Wananchi.

Upvote
1