Chulumeshy
Member
- Jul 27, 2022
- 17
- 11
Kama wote tutakuwa sawa chini ya sheria na hakuna hata mmoja atakayekuwa juu ya sheria hiyo ndiyo itakapokuwa nchi yenye misingi ya kisheria.
Sheria inatakiwa imuhusishe kila mtu ndani yake ukiingiza na serikali ndani yake kwani serikali pia imebeba watu inaowatumikia katika kufanya kazi katika mihimili wake.
Maneno hayo yameongelewa na Fatuma Karume ambaye ni mwanasheria wa kitanzania na wakili wa kujitegemea ambaye aliwahi kuwa Rais wa chama cha Wanasheria Tanganyika katika kipindi cha mwaka 2018 hadi 2019.
Yamezungumzwa katika mkutano wa Miaka 30 ya Mfumo wa Vyama Vingi, uliyosimamiwa na Tanganyika Law Society Jumamosi ya tarehe 30 mwezi wa 07/ 2022.
Kwamba mahakama inatakiwa ipewe uhuru wa kufanya kazi zake kama mahakama na kuweza kutoa maamuzi yake kama mahakama lakini kulingana na namna moja au zaidi imepelekea mahakama kuwa chombo dhaifu cha watu kwenda kuzidai haki zao na hii ni kutokana na baadhi ya watu wenye cheo na mali kutumia mahakama kwa ajili ya kupotosha haki na kufanya haki za watu kutokutendeka kwa uaminifu jambo linalofanya watu wengi kuogopa kuwasilisha madai yao katika mahakama kwa imani ya kuwa hawataweza kuipata haki yao.
Hivyo basi ili kuleta Uhuru wa mahakama katika masuala ya Kidemokrasia ni lazima Mahakama iweze kuchagua mirengo yake mwenyewe mfano, mahakama yenyewe kuchagua Chief Of Justice badala ya Rais jambo linalompa mamlaka Rais kuweza kubadisha uongozi wa Chief Of Justice kama hatoridhika nae na pia huyohuyo ndiye anayehusika na masuala yote ya uchaguzi hivyo kwa namna moja au nyingine inapelekea kutokuwa na ule uhuru wa moja kwa moja katika uchaguzi.
Pia katika Rule of Law in Democraacy tunatakiwa tuangalie vitu mbalimbali kama;
-Equality
Kwamba lazima kuwe na usawa mfano katika taasisi mbalimbali wanawake kuajiriwa katika vyeo vikubwa vimekuwa kwa uchache sana hata katika taasisi zinazohisika na sheria hivyo ni lazima kuwe na equality kote.
Hata katika watu wenye uhitaji maalumu pia kuweze kuwa na usawa katika demokrasia yao.
-Political tolerance (uvumilivu wa kisiasa)
Kuwe na heshima baina ya watu
Sauti za wanyonge zitiliwe maanani.
-Accountability(uwajibikaji)
-Uwazi (Transparency)
-Kuwe na chaguzi huru (Free nad Fair Election)
-Uhuru wa kiuchumi(economic freedom)
-Control the Abuse of Power
-Haki za Kisheria
-Kukubali matokeo ya Uchaguzi
Kusimamia haki za kibinadamu
Ikumbukwe
Majaji na Mawakili hawaruhusiwi kuwa katika chama chochote cha kidemokasia.