SoC03 Kuwe na Wahasibu Maalumu katika Sekta ya Afya

SoC03 Kuwe na Wahasibu Maalumu katika Sekta ya Afya

Stories of Change - 2023 Competition

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
2,087
Reaction score
3,156
UTANGULIZI
Kwa miaka mingi sasa sekta ya afya, masuala ya usimamizi wa fedha na kihasibu, manunuzi na mengineyo yamekuwa yakisimamiwa wa wahasibu ambao niwa kawaida kwa ajili ya biashara za uzalisha ambao wanatambulika kama “CERTIFIED PUBLIC ACCOUNTANT (CPA)”, kwa namna moja ama nyingine kiuhalisia hawana weledi wa kusimamia na kushughurikia masuala ya fedha na kihasibu yanayohusu afya kwa sababu;
  • Kanuni za kihasibu ambazo wao wanatakiwa kuzifuata zinakinzana na mfumo wa uendeshaji shughuri za kiutendaji katika sekta ya afya kama manunuzi na marekebisho ya vifaa tiba.
  • “CPA” wao wanatambua kwamba Fedha ni kipimo cha ukuaji wa uchumi, ama fedha ni kipimo cha maendeleo ya kiuchumi, wakati masuala ya kihasibu katika sekta ya afya yanatambua kama Fedha ni kichocheo cha uzalishaji katika uchumi.
  • Uandaaji wa bajeti ya kihasibu katika masuala ya afya na ile katika uhasibu wa kawaida unatofautiana.
  • Mfumo wa uendeshaji wa sekta ya afya ni tofauti na mfumo wa uendeshaji katika biashara nyingine hivyo kufanya mahitaji ya gharama za uendeshaji kutofautiana.
  • Gharama za uendeshaji wa biashara zinazohusisha uhasibu wa kawaida uwasilishwaji wake ni tofauti na gharama za za kihasibu katika masuala ya afya.
Maana yake ni kwamba wahasibu wanaotumika katika sekta ya afya wanatumia kanuni na miongozo ambayo haiendani na inakinzana na mahitaji ya sekta husika, kitu kinachopelekea kuwa na makosa mengi ya kihasibu na kiutendaji kama vile marekebisho ya vifaa nje ya wakati, ucheleweshwaji wa manunuzi wa vifaa tiba muhimu ama madawa kwa sababu tu kanuni za kihasibu zinazotumika zinakindhana na uhalisia wa sekta husika.

NINI KIFANYIKE
Serikali iunde bodi ya usimamizi wa masuala kihasibu katika sekta ya afya itakayotambulika kitaalamu "TANZANIA COST ACCOUNTING STANDARD BOARD (TCASB)” ambayo itakuwa chini ya wizara ya afya na itakuwa huru na itasimamia masuala yote ya kihasibu na fedha yanayohusu sekta ya afya ikiwemo;
  • Kutunga kanuni za kihasibu zitakazotumika na wahasibu katika sekta ya afya
  • Kutunga miongozo ya kihasibu katika sekta ya afya.
  • Kufanya tathmini ya mtiririko wa mgawanyo wa fedha na mahitaji katika hospitali zote kama ulifuata kanuni zilizowekwa.
  • Kutunga sera za kihasibu katika sekta ya afya
  • Kufanyia marekebisho miongozo na kanuni za kihasibu katika sekta ya afya.
  • Kutoa mafunzo maalumu ya kihasibu yanayohusu sekta ya afya.
  • Kutoa leseni ya uhasibu maalumu katika sekta ya afya.
  • Kukagua wahasibu katika sekta ya afya kama ni maalumu na wamesajiliwa nk.
Sambamba na hilo mhasibu maalumu katika sekta ya afya yeye atambulike kama “CERTIFIED COST ACCOUNTANT (CCA)” au “CERTIFIED MANAGERIAL ACCOUNTANT (CMA)”

Katika sekta ya afya wakaguzi wote wa ndani na nje ni lazima awepo mhasibu mwenye leseni ya bodi ya uhasibu katika sekta ya afya.

MUUNDO WA BODI
Bodi iundwe na wajumbe wasiopungua na wasiozidi watano ambao watapatikana kwa mujibu wa sheria itakayotungwa na bunge,wajumbe hao itahusisha;
  • Mganga mkuu wa serikali ambaye atakuwa ndiye mwenyekiti wa bodi
  • Afisa ugavi mkuu wa serikali
  • Mwanasheria wa masuala ya kihasibu na fedha aliyesajiliwa.
  • Mjumbe mmoja kutoka ofisi ya Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali.
  • Mwenyekiti wa bodi ya wahasibu wa kawaida.
FAIDA YA KUWA NA BODI
  • Itatengeneza mfumo imara wa usimamizi wa masuala ya kihasibu katika sekta ya afya kupitia sera bora na miongozo.
  • Itahakikisha ubora na uimara katika maendeleo ya sekta ya afya.
  • Itaanda wataalam wenye miiko na miongozi imara ya kihasibu inayohusu afya.
  • Itasaidia kuondoa vikwazo vilivyokuwa vinakwamisha ubora wa utendaji kazi katika sekta.
NAMNA WAHASIBU WATAPATIKANA
Serikali kupitia wizara ya elimu ianzishe kozi ya uhasibu katika sekta ya afya katika ngazi ya astashahada, shahada, na shahada ya uzamili, kwa watakao soma shahada ya uzamili lazima wawe na shadada ya uhasibu, ugavi ama afya.

Baada ya kuhitimu masomo yao watalazimika kufanya mtihani wa bodi iliyoundwa na watakaofaulu mtihani huo watapewa leseni itakayowaruhusu kufanya kazi kama wahasibu katika sekta ya afya.

Kwa ambao ni wahasibu wa kawaida na wameajiriwa katika sekta ya afya na wanamuda mfupi tangu waajiriwe watalazimika kwenda kusoma ili wapate mafunzo na kuwa na leseni, kwa wale ambao ni wa muda mrefu na wamekaribia kustaafu watapewa mafunzo mafupi ambayo yataandaliwa na bodi na kufanya mtihani, watakao faulu wataendelea na majukumu yao na watakao feli watalazimika kurudia mafunzo na mtihani.

Sambamba na hilo serikali itangaze mara moja baada yakukamilisha mchakato kwamba kitengo cha fedha, manunuzi na uhasibu katika sekta ya afya ni lazima kisimamiwe na wataalumu maalumu wa masuala hayo katika sekta husika.

FAIDA YA KUWA NA KUTUMIA WAHASIBU MAALUMU KATIKA SEKTA YA AFYA
  • Huzingatia kanuni za uzalishaji na utoaji huduma kwa haraka.
  • Hupunguza mrundikano wa vifaa ambavyo vinahitaji marekebisho ya haraka.
  • Hupunguza mzunguko katika uidhinishwaji wa fedha kwa ajili ya manunuzi ama marekebisho na malipo.
  • Huzuia kukwama kwa huduma muhimu za kiafya.
  • Huakikisha uwepo wa mahitaji yote muhimu katika kituo cha afya ama hospitali.
  • Huzingatia utoaji wa huduma bora katika sekta ya afya.
  • Hupunguza ubadhilifu ama upotevu wa fedha za umma.
Kwa dhama za sasa ili sekta ya afya iweze kuendesha shughuri zake na kutoa huduma kishindani halinabudi kufuata kanuni za usimamizi wa sekta husika, hivyo ni rahi yangu serikali kuchukua hatua dhidi ya suala hili ili kuendana na matakwa ya ubora katika sekta hii.
 
Upvote 9
Sawa sawa mkubwa,hata kama usipochukua milion 2kama mwaka jana ulichokiandika kikifanyiwa utekekezaji kitakuwa na manufaa sana
 
akili mingi, asante chief. nyie ndo wale samia alisema mfanyiwe vetting muingie kwenye tume ya mipango.
natamani andiko hili liwafikie wakubwa mawazo haya ni very helpful
 
Najaribu kujiuliza, kwani nchi zingine wanafanyaje? Maana haya mambo ya bodi kwetu ni mengi sana, mwishowe naona kila kitu kitakuwa na bodi yake.

Kama ni lazima kwanini isiwe section chini ya bodi iliyopo ya uhasibu?
 
Sawa sawa mkubwa,hata kama usipochukua milion 2kama mwaka jana ulichokiandika kikifanyiwa utekekezaji kitakuwa na manufaa sana
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] weee, watu mnafuatilia, ahsante sana lengu sio mimi kushinda bali Taifa langu kushinda, kuna chapisho nyingine pia unaweza kuzipitia.
 
Najaribu kujiuliza, kwani nchi zingine wanafanyaje? Maana haya mambo ya bodi kwetu ni mengi sana, mwishowe naona kila kitu kitakuwa na bodi yake.

Kama ni lazima kwanini isiwe section chini ya bodi iliyopo ya uhasibu?
Ni kwa namna yeyote ile itakavyo kuwa lakini kwangu haya ni maoni, USA na EUROPE wanatumia huu mfumo nilioupendekeza.
 
Sifa za kusoma hyo koz Ziwe Zipi? Kwa mtazamo wako aliyesomea taaluma ya afya angefaha kusomea hyo fani pia ?
 
Sifa za kusoma hyo koz Ziwe Zipi? Kwa mtazamo wako aliyesomea taaluma ya afya angefaha kusomea hyo fani pia ?
Naam, nimeelezea katika andiko hapo kwamba waliosoma public accounting, na kozi nyingine za afya wanaweza kujiunga, mwenye bachelor yoyote ya kozi ya afya ataweza kujiunga na kozi hiyo kwa level ya masters mwenye diploma kwa level ya bachelor
 
Back
Top Bottom