king Mazee
New Member
- May 10, 2024
- 3
- 0
Kufikia Tanzania tuitakayo ni lazima kuhakikisha kuwa Vyanzo vikuu vya maji vinatunzwa na kulindwa ipasavyo kwakuwa Nchi inaweza kuweka malengo pamoja na mipango madhubuti kabisa lakini bila mpango mkakati juu ya suala la vyanzo vya maji ikashindwa kufikia malengo kwakuwa vyanzo vya Maji katika Nchi yetu ni sawa na mzunguko wa damu katika mwili wa binadamu, kwa mfano tumeshuhudia mara nyingi watu wakipoteza maisha pamoja na mali zao, sio Mijini wala Vijijini na kufanya nguvu kazi ipungue pengine ndiyo ingeweza fanikisha shauku ya Tanzania Tuitakayo katika Miaka 5 mpaka 25 ijayo na kwa kiasi ambacho kwa namna moja ama nyingine maendeleo ya Nchi kukawia kwakuwa badala ya kuendelea na mambo mengine serikali inaamua kuweka nguvu kwenye majanga ambayo pengine kungelikuwa na mpango mkakati mzuri yangeweza kuepukika.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiamua kufanya yafuatayo itaweza chochea kupelekea Tanzania kufikia ya kutamanika katika ukuaji wake kwenye mambo yote pamoja na ya Maendeleo zaidi kwa Miaka 5 mpaka 25 ijayo
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiamua kufanya yafuatayo itaweza chochea kupelekea Tanzania kufikia ya kutamanika katika ukuaji wake kwenye mambo yote pamoja na ya Maendeleo zaidi kwa Miaka 5 mpaka 25 ijayo
- Kuweka sheria juu ya vyanzo vya maji kama Mito, kuzuia kujenga maeneo hayo. Katika Nchi hii maeneo hatarishi yanajulikana, kipindi cha mvua kwa Mfano baadhi ya maeneo ya Dar Es Salaam yanaonekana kuathirika zaidi nahii inatokana na uwepo wa mito ambayo njia zake kwa sasa ni makazi ya watu, sasa haya maeneo yanajulikana lakini kwa tamaa za watu wachache waliopewa mamlaka kuamua kuyauza maeneo hayo bila kujali utu na upendo kwa wengine ijapokuwa wanajua kuwa maeneo hayo sio rafiki kwa mwanadamu. Iwapo sheria itawekwa kuwa hakuna maeneo haya kuuzwa wala kujengwa makazi ya watu na badala yake kuweza kuweka mpango mkakati wa namna ya kuhifadhi vyanzo hivi kwa utaratibu.
- Kuwekwa sheria kwa kiongozi yeyote atakaye chukua rushwa kwaajili ya kuuza na kuwapa ruhusa watu kuweza kujenga maeneo hayo kuchukuliwa hatua. Hii itasaidia kupunguza maafa yanayotokana na watu kusombwa na mito na kupoteza vitu vyao kwakuwa watu hao unakuta wamenunua ardhi bila kuambiwa kuhusu maeneo hayo kuwa ni hatarishi na kwakuwa watu walio wengi waliopewa mamlaka ya kusimamia wanaangalia mbele pesa kuliko utu na upendo kwa wenzao na kuwafanya wenzao kuingia katika shida, sheria iwekwe kwaajili ya watakao husika na uuzaji maeneo hayo.
- Maeneo hayo ni vyema yatengwe na kujengewa panapowezekana,Ninachokijua ni kwamba Serikali ikiamua jambo lake haiwezi kushindwa, kama mbuga za wanyama zimefanikiwa kutengwa na hata jambo lolote lile kama hili linawezekana pia, hii itapunguza athari nyingi pamoja na matatizo yatokanazo na athari hizo
- Kuwe na maeneo kila Mkoa na ikiwezekana kila Mtaa hata kama ni kijisehemu kidogo ambapo Serikali itatenga kwaajili ya upandaji Miti. Miti au Mistu huleta Mvua ambacho nimojawapo ya chanzo cha Maji, kwa maana nyingine Miti au Misitu hutegemea Mvua na Mvua hutegemea Miti au Misitu . Serikali ikiamua kila Mtaa kwa kuwa una Wajumbe, yakatengwa maeneo kwaajili ya upandaji Miti, ikawepo sheria kwamba kila Mwananchi wa eneo hilo ahakikishe amepanda Mti katika eneo lililotengwa kwaajili ya Miti au Mistu kupitia kwa Mjumbe au Wajumbe wa eneo hilo. Hii itasaidia kulinda Ardhi na kuwezesha hali nzuri ya hewa ya eneo hilo na kwa vile itakuwa ni kwa Nchi nzima mfumo huo utafanyika kote. Hii itachangia na kuchochea watu katika ufanyaji kazi wa watu wafanye kazi katika Mazingira mazuri na kwa uimara zaidi kwakuwa hewa safi itakuwa ya kutosha kulingana kwamba hali mbaya ya hewa inaongezeka kila kukicha kulingana na mfumo wa Maisha na Ongezeko la viwanda kulingana kuwa kumekuwa na kasi kubwa sasa ya wawekezaji kutoka nje na wa ndani, hivyo tunahitaji sana hatua hii ya upandaji miti au misitu iweze kuchukuliwa na kutendewa kazi kuweza chochea Maendeleo ya Taifa la Tanzania.
- Dunia inaenda kidigitali zaidi, ni vyema sasa kuenenda kiteknolojia zaidi, kwa mfano kuna ukataji na uharibifu mwingi wa miti na uharibifu huo unajulikana katika maeneo hayo, nivyema sasa Mamlaka husika kuenenda kiteknolojia ili ikiwezekana maeneo hayo yaweze kuwa yanaonekana hata mtu awapo Mjini katika Ofsi awe na uwezo wa kujua kuwa asaivi kwenye Msitu kuna moja mbili. Kama Sehemu zingine zinaweza kuwekewa system nakuonesha kila kitu kinachoendelea katika eneo hilo, kwanini sehemu zenye vitu muhimu pashindikane ?., kama Bajeti inatengwa kwaajili ya kitu flani, inawezekana pia Bajeti ikawepo kwaajili ya hiyo System kwakuwa kwa kufanya hivyo kutapunguza rushwa ambacho ndio chanzo kikubwa kinakwamisha Maendeleo
- Mwisho kabisa nipende kushauri kuwa, inawezekana tukalinda vyanzo vyam Maji na vyanzo vingine vyote. Kuenenda kiteknolojia kuwe katika sehemu zote, katika Sekta zote, kwa kuweka Mifumo kwa kutumia Wataalamu mbalimbali wa masuala ya teknolojia, mifumo ya kisasa ya kuonesha chochote kinachoendelea katika eneo husika, iwe ni maeneo ya migodi, maeneo ya misitu na maeneo mengine ya vyanzo vya Maji pamoja na maeneo yeyote ambayo kupitia hayo kuna upotevu wa pesa nyingi ambao unakwamisha Maendeleo ya Taifa hili, kwakufanya hivyo kutapunguza rushwa katika watu wanao uza maeneo ya vyanzo vya Maji huku wakifahamu kuwa maeneo hayo siyo rafiki kwa makazi ya wanadamu.
Upvote
1