Katika mazingira ya kawaida kuweka tinted sio tatizo na yapo baadhi ya magari huuzwa yakiwa nayo kutokata na kazi ya msingi iliyokuwa inafanywa na gari husika
Ila sasa huku ULIMWENGU WA TATU imekuwa changamoto pale watu wenye nia ovu wanapotumia huo mwanya kufanya uhalifu
Mfano:
1. Watekaji wote waliotajwa kwenye vyombo vya habari wakiwa na gari/magari wametumia magari yenye tinted hadi kioo cha mbele
2. Wezi vya vibanda vya miamala wengi waliotajwa wametumia magari kama hayo
3. Majambazi wote wanaotumia magari wote wanatumia muanya huo huo
4. Inapelekea uoni hafifu wakati wa kuendesha na kuongeza uwezekano wa kufanya makosa au niseme kupata ajali barabarani
Fikiria mtu amekuja na kupaki gari karibu na ofisi yako au hata nyumbani kwako na limewekwa tinted hadi kioo cha mbele; huwezi kujua kuna mtu na nia yake pengine ovu ya kukudhuru au kukuibia
Tukiweka kwenye mizani; hasara za kuweka tinted Kioo cha mbele ni nyingi kuliko faida HIVYO ipo haja ya mamlaka husika kuliangalia hili suala hasa kwa usalama wa watu na mali zao