Kuwekwa mahabusu upelelezi haujakamilika

Kuwekwa mahabusu upelelezi haujakamilika

kluger

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2016
Posts
2,093
Reaction score
1,899
Wataalamu wa Sheria, salaamu kwenu,

Naomba kufahamu suala tajwa hapo juu.
Nimekuwa nikisikia na kusoma mashauri mbali mbali ya kesi zilizopo mahakamani, kuwa kesi imeahirishwa watuhumiwa wanarudishwa rumande upelelezi haujakamilika.

Na watuhumiwa wanakuwa mahabusu/rumande zaidi ya mwaka mmoja.

Je hili limekaaje kisheria? Ni haki kwa mtuhumiwa kukamatwa ili hali upelelezi haujakamilika?

Kwa nini upelelezi usifanyike kwanza kabla ya kumkamata mtuhumiwa?

Naomba ufafanuzi kidogo katika hili.

Ahsanteni Sana.
 
Hilo la kukamatwa na upelelezi ukaendelea linawezekana.
Tatizo ni pale mtuhumiwa anaponyimwa dhamana ikiwa ni makosa yanayodhaminika kisheria.

Chukulia mfano umelala na mkeo na akakutwa amefariki kesho yake na wewe kukimbilia kusikojulikana. Utakapokamatwa na ni lazima polisi ifanye upelelezi wa kutosha kujiridhisha na mazingira ya tukio na uhusika wako kama mtuhumiwa ili kuwa na ushahidi wa kutosha kuendesha kesi.

Wewe mwenyewe unakuwa ni sehemu ya upeleiezi huo.
 
Kwanni mahabusu zisiwe nyumba tu za hali ya kawaida na mazingira yasiyohatarisha afya za watuhumiwa?? Kwann mahabusu wanalundikwa kama magunia?? Kwann wasiwekwe sehemu zinazokidhi afya zao?? Huu ni uonevu mkubwa sana.
 
Nimefikiria sana kuhusu hizi sheria zinazozuia mtuhumiwa/mshukiwa kunyimwa dhamana wakati mahakama haijathibitisha kama ni mkosaji kulingana na sheria.

Vulevile mtuhumiwa anakaa ndani kwa miaka hata saba alafu anakuja kushida kesi kweli ni uonevu.

Kuna sheria zinatumika kukandamiza baadhi ya watu especially kama kuna ugomvi binafsi kati ya kiongozi na muhusika kwasababu hazina dhamana mfano mzuri ni UTAKATUSHAJI WA PESA.

Hizi sheria hazitendi haki kwasababu zinamlazimisha muhusika kukiri makosa ili tu atoke maana muda ambao kesi inaendeshwa na yeye yupo ndani ni zaidi ya MIAKA SABA NA KUENDELEA wakati akikiri makosa KIFUNGO CHAKE NI MIAKA MITANO AU FAINI YA TSH MILIONI 200.

Kwahiyo sheria zetu bado ni kandamizi, zipo kwa ajili ya maslahi mapana ya WATAWALA.

So sad.
 
Back
Top Bottom