Wataalamu wa Sheria, salaamu kwenu,
Naomba kufahamu suala tajwa hapo juu.
Nimekuwa nikisikia na kusoma mashauri mbali mbali ya kesi zilizopo mahakamani, kuwa kesi imeahirishwa watuhumiwa wanarudishwa rumande upelelezi haujakamilika.
Na watuhumiwa wanakuwa mahabusu/rumande zaidi ya mwaka mmoja.
Je hili limekaaje kisheria? Ni haki kwa mtuhumiwa kukamatwa ili hali upelelezi haujakamilika?
Kwa nini upelelezi usifanyike kwanza kabla ya kumkamata mtuhumiwa?
Naomba ufafanuzi kidogo katika hili.
Ahsanteni Sana.