Sijui Kama najua mengi, lakini najaribu kusoma kila siku kidogo kidogo cryptocurrency news, Telegram forums on cryptocurrency, n.k. Namna hii naweza kwa muda kuwa na wazo Fulani kuhusu trends, na kuangalia kama kwamba crypto coins Kama Bitcoin au Ethereum zitakuwa juu zaidi au la mwisho wa siku. Kwa hiyo, kwanza kabisa, GET INFORMED. Usiweke pesa yapo kwa wakala wowote bila wewe kuelewa kwanza soko lenyewe.
Pili, kanuni muhimu sana usiwekeze pesa yako yote. Afadhali kuwekeza dola mia Kama ni hizo unazoweza kuwekeza kuliko usd50,000 ulizozipata kwa kuweka nyumba, gari, na maisha ya familia yako rehani.
Tatu, BE RATIONAL, NO EMOTIONAL. Panga vizuri. Kwa mfano, badala ya kuwekeza kwenye bitcoin tu, weka pesa kwenye Bitcoin na kwenye Ethereum, hata kweye crypto coins Nyingine Kama Ripple. Kwa kizungu, build your eggs´ basket. Nunua kidogo Bitcoin, kidogo Ethereum, na kadhalika, namna hii risk yako ipo less ya kupoteza pesa yako.
Nne, haiwezekani kutabiri kabisa cryptocoins zitapanda namna gani na kwa kipindi gani, wala kujua faida yako itakuwa asilimia ngapi. This is a speculative market. Ndiyo maana daima uwe informed. Trend ya mwaka huh 2017 inatabiri Bitcoin bado inaanza kupanda, maana Kama leo ipo usd5776 itafika usd6000, itabaki hapo, itashuka (watu watauza kwa kuchukua faida), itapanda tena juu ya 6000,na kutoka hapa itaendelea kwenda juu. Na 2018 hivo hivo. Angalia sijasema itakuwa hivo, hapana, ila nimesema kwamba trends zinaonyesha itapanda. Lakini kwa sababu ni speculative market inaweza pia kuwa affected na black swans (kwa mfano vita Korea, au a new economic crisis, au matatizo ya siasa au vita).
Kwa hiyo, ukitaka kuwekeza, be informed, be rational, be aware, na uwe tayari kushinda na kushindwa. Wewe mwenyewe unaweza kununua crypto yako kwenye mtandao, bila kutumia kampuni kama si kampuni unaponunua au unapouza crypto. Unakuwa na crypto wallet ya kwako binafsi. Unaiacha bila shida kwa muda kwa mfano wa mwezi moja. Hapo unaangalia thamani ya crypto ipoje. Pengine umewekeza usd 1000 na sasa thamani ya crypto kwenye wallet yako ni 3000, basi uza 1000, rudisha pesa yako uliowekeza mikononi mwako, na uendelee kuoperate na crypto ya thamani ya 2000. Uwe Patient na uache egg basket yako ikue na ikue. Ukiona crypto inafika kwenye roof Fulani uza kidogo, upate faida, ukiona wakati fulani bei imeshuka kwenye bei correction, nunua kidogo tena. Unamanage funds mako namna hii. Si lazima uwe msomi wa Finance, lazima kila siku uwe na common sense. Uwe tayari pia kupoteza pesa uliowekeza.
Nafikiri nimekusaidia kidogo. Naonya tena, lakini, kwamba mimi si authority wa soko la crypto, ila najaribu kupata faida kwa kuwa informed na kuangalia trends, na kutumia common sense, na kufanya rational no emotional decisions. Anza na kusoma kila siku
www.coinmarketcap.com kwa mfano. Angalia trends. Kwa kupata news,
www.blockchaincompany.info (naipenda sababu ukiwa member bure wanakupa free assigned locked tokens, na hizo tokens watakapozilaunch zitakuwa unlocked na na thamani kwenye soko la tokens) hapa unapata habari mbalimbali pia wanakuconnect moja kwa moja kwa Bloomberg (
www.blockchaincompany.info/tv). Ni kawaida mwanzoni faida yako iwe kidogo au upoteze pesa kidogo. Unapoendelea kukazana na kujifunza faida inakuja haraka zaini kwa sabbat tayari unajua wapi na namna gani kuoperate investment yako.