SoC04 Kuwepo na uwiano: Uchumi wa kati wa nchi uwe pia wa kati kwa wananchi

SoC04 Kuwepo na uwiano: Uchumi wa kati wa nchi uwe pia wa kati kwa wananchi

Tanzania Tuitakayo competition threads

Story Zaukweli

New Member
Joined
May 17, 2024
Posts
4
Reaction score
4
Utangulizi;
Elimu, kilimo, afya na tekinolojia vyote huongeza ujumuishi wa uchumi wa Kati wa nchi uwe pia wa kati kwa wananchi,Tekinolojia katika madini kama chuma na madini ya vito, tuweze kuongeza thamani ya madini yetu wenyewe na kuacha kuuza mali ghafi, tujenge viwanda vya kuongeza thamani, bidhaa zetu ziwe na ubora unaohitajika katika soko au masoko ya nje ya nchi.

Katika kilimo wananchi wanoahitaji kulima wawezeshwe dhana Bora, elimu, mtaji na ardhi.
Pamoja na BBT kuwepo lakini bado ardhi kubwa Sana inayofaa kwa kilimo haitumiki ikingoja wawekezaji, Tanzania tuitakayo ni ile inayoweza kuwabadilisha wakulima wadogo kuwa wakulima wakubwa, wawekezaji wadogo kuwa wawekezaji wakubwa, serikali inahitajika kuwakuza wakulima wadogo ki elimu na namna kilimo Bora chenye tija kinavyofanywa. Elimu Kama mbegu Bora za kilimo zinazoweza kuhimili ukame, magonjwa na kuzaa kwa wingi ili mkulima aweze kupata kingi katika eneo dogo. Dhana kama vile mashine ya kukaushia mazao kwa ajili ya kuyatunza pasipo kuharika pale mkulima anapohitaji kusubiri bei ya soko itakapo kaa sawa.

Tukuze tekinolojia iweze kuwafanya wataalamu wetu kuwa wabunifu.
Hakuna iliyoendelea bila ukuaji wa tekinolojia, Kwanza tekinolojia ndio chanzo cha ukuaji wa sekta yoyote, tuwajengee wataalamu wetu iwezo wa kuwa wabunifu na watatuaji wa matatizo ya wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, waweze kutengeza madwa, na machine ndogo ndogo zitakazo warahisishia wananchi katika kilimo na sekta zingine.

Kila eneo la bahari na maziwa makubwa kuwe na kiwanda vya kuchakata samaki.
Katika Kila sehemu shuhuli za uvuvi zinapo endelea kuwepo na angalau kiwanda kidogo Cha kuchakata samaki na kupelekwa katika soko la nnje, inaweza kuwainua wavuvi wetu kuliuchumi na angalau kukuza kipato chao cha kila siku na kuweza kukidhi mahitaji yao binafsi na kutunza familia zao. Wizara na mabalozi wanao iwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali wajadiliane namna ya kuwatafutia wadau wa kilimo na uvuvi masoko nnje ya nchi ili kuwezesha sekta ya kilimo na uvuvi kukua katika nchi yetu na kusaidia kukuza uchumi wa nchi yetu na uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.

Kuharakisha uchimbaji wa mafuta ili kurahisisha uzalishaji katika viwanda vyetu.
Kwa sababu sekta ya viwanda hutegemea Sana dizeli na usafirishaji hutegea Sana petroli, uchimbaji wa mafuta utarahisisha sana uzalishaji katika viwanda vyetu kwa kupunguza gharama za uzalishaji na usafirishaji na kuongeza faida kwa wananchi na kuwahahakishia soko kwa wale wakulima na kipato kwa wale wanaofanya Kazi katika viwanda hivyo.
Pia kuharakisha uchimbaji wa mafuta kutaleta fedha za kigeni katika nchi yetu na kukuza uchumi wetu, utakao rahisisha na kuboresha Sekta mbalimbali kama umeme, afya, maji nk.

Kutenga maeneo ya malisho kwa wafugaji na maeneo ya kilimo kwa wakulima.
Ili kuepuka harasa za kulishiwa mazao na kuuwawa kwa mifugo na watu kwenye mapigano kati ya wakulima na wafugaji, yatengwe maeneo maalumu kwa ajili ya shuhuli za kilimo na maeneo kwa ajili ya malizo.
Wafugaji wafundishwe ufugaji wa kisasa katika eneo dogo kugawanya vitalu na kupanda nyasi, ili kuwe na mzunguko wa mwaka mzima kugawanywe vitalu vinne vya kulishiwa kwa miezi mitatumitatu kwa mzunguko wa mwaka mzima. Ili kuepusha malisho kuisha na kukosa sehemu ya kulisha katika wakati wa kiangazi.
Wafugaji washauriwe kupunguza mifugo yao kutokana na ardhi iliyopo, ili kuepuka kukosa sehemu ya kulishia na kwenda kuvamia mashamba ya wakulima. mashamba na malisho yanatakiwa yasipakane ili kuepuka mzozo.

Tekinolojia yenye ubunifu, ibuniwe ili kuzuia tembo kuharibu mazao ya wananchi.
Kwa kufanya ubunifu Kama kubuni Uv kamera, iliyo na spika yenye sauti kubwa ambayo itakua automatiki kugundua umbo la mnyama ambaye ni tembo, na kwenye umbali wa mita Mia ha mia mbili kabla ya tembo kuikaribia ipige ving'ora, na sauti zote zinazo tumika kuwafukuzia tembo zihifadhiwe kwenye kamera hiyo.
Kamera hizi zifungwe katika mipaka ya hifadhi iliyo karibu na makazi ya watu sehemu ambazo hifadhi hupakana na mashamba ya wananchi.

Wavuvi wapewe au wakopeshwe vizimba ili kuendeleza maisha yao pale maziwa yanapo pumzishwa.
Ili kuto dhoofisha uchumi wa wavuvi pale mabwawa makubwa na maziwa yanapofungwa, serikali wanapaswa wajue namna ya kuwawezesha wavuvi wasitegemee tu maziwa na mabwawa tu Bali wapate mbinu ya kufuga kisasa kutumia vizimba.

Bima iwe bure fedha ipatikane kwenye makapuni ya kubeti.
Serikali iongeze kodi kwenye makapuni ya kubeti ili bima ya afya iwe bure, na hata matibabu na dawa viwe bure ili kuwa rahisishia wananchi huduma, maana wananchi wakiwa na uhakika wa afya zao, uchumi wao na wa nchi utakua na uwiano.

Wahitimu wa vyuo vya ufundi waajiriwe moja kwa moja wanapohitimu.
Serikali iwahamasishe wawezekezaji kuwekeza zaidi katika sekta ya viwanda ili kuwezesha mabadiliko ya mfumo wa elimu kuwa na tija.

HITIMISHO;
Ili kuendeleza mbele taifa letu elimu, tekinolojia, siasa, kilimo, afya na vingine vingi kwa jumla yake huleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na hatimae kwa taifa zima. Hivyo mkazo uwekezwe katika kuendeleza sekta zote muhimu ili tuendane na ukuwaji wa tekinolojia, afya , kilimo bora, siasa safi na demokrasia bora. ili uchumi wa nchi uendane na wa wananchi.
 
Upvote 4
Kuharakisha uchimbaji wa mafuta ili kurahisisha uzalishaji katika viwanda vyetu.
Kwa sababu sekta ya viwanda hutegemea Sana dizeli na usafirishaji hutegea Sana petroli, uchimbaji wa mafuta utarahisisha sana uzalishaji katika viwanda vyetu kwa kupunguza gharama za uzalishaji na usafirishaji na kuongeza faida kwa wananchi na kuwahahakishia soko kwa wale wakulima na kipato kwa wale wanaofanya Kazi katika viwanda hivyo.
Kujitosheleza kinishati ni muhimu kuendesha injini za uchumi, ahsante.

Wafugaji wafundishwe ufugaji wa kisasa katika eneo dogo kugawanya vitalu na kupanda nyasi, ili kuwe na mzunguko wa mwaka mzima kugawanywe vitalu vinne vya kulishiwa kwa miezi mitatumitatu kwa mzunguko wa mwaka mzima. Ili kuepusha malisho kuisha na kukosa sehemu ya kulisha katika wakati wa kiangazi.
Wafugaji washauriwe kupunguza mifugo yao kutokana na ardhi iliyopo, ili kuepuka kukosa sehemu ya kulishia na kwenda kuvamia mashamba ya wakulima.
Hapa nataka nichukue nusu, nikubali kuwahamisha mizunguko ya miezi kadhaa mifugo, lakini sio kupunguza idadi. Tuongeze idadi tuzalishe nyama na mazao ya mifugo ya kutosha hadi soko la nje.
Tena mtindo ulopendekeza wa kuwazungusha unaweza hata kufaidisha kuzitumia baadhi ya mbuga na hifadhi kuwazungusha humo makundi kwa makundi. Na bahati nzuri hiyo imeonekana kuwa ni njia bora kabisa ya uhifadhi wa mazingira.

View: https://youtu.be/vpTHi7O66pI?si=5t0va2RHU0_r1CHk

Bima iwe bure fedha ipatikane kwenye makapuni ya kubeti.
Serikali iongeze kodi kwenye makapuni ya kubeti ili bima ya afya iwe bure, na hata matibabu na dawa viwe bure ili kuwa rahisishia wananchi huduma, maana wananchi wakiwa na uhakika wa afya zao, uchumi wao na wa nchi utakua na uwiano.
Hahahahaaaaah we jamaa 😁😁, je hatutakuwa tunatoa fedha kwenye kundi moja na kupeleka kwingine bila kuwawajibisha wahusika. Hata hivyo bima ya bure labda iishie kwa watoto tu. Watu wazima inapaswa wawajibike na afya zao.

kuendeleza mbele taifa letu elimu, tekinolojia, siasa, kilimo, afya na vingine vingi kwa jumla yake huleta maendeleo ya mtu mmoja mmoja na hatimae kwa taifa zima. Hivyo mkazo uwekezwe katika kuendeleza sekta zote muhimu ili tuendane na ukuwaji wa tekinolojia, afya , kilimo bora, siasa safi na demokrasia bora. ili uchumi wa nchi uendane na wa wananchi.
Hakikaaa, ahsante
 
Kujitosheleza kinishati ni muhimu kuendesha injini za uchumi, ahsante.

Hapa nataka nichukue nusu, nikubali kuwahamisha mizunguko ya miezi kadhaa mifugo, lakini sio kupunguza idadi. Tuongeze idadi tuzalishe nyama na mazao ya mifugo ya kutosha hadi soko la nje.
Tena mtindo ulopendekeza wa kuwazungusha unaweza hata kufaidisha kuzitumia baadhi ya mbuga na hifadhi kuwazungusha humo makundi kwa makundi. Na bahati nzuri hiyo imeonekana kuwa ni njia bora kabisa ya uhifadhi wa mazingira.

View: https://youtu.be/vpTHi7O66pI?si=5t0va2RHU0_r1CHk

Hahahahaaaaah we jamaa 😁😁, je hatutakuwa tunatoa fedha kwenye kundi moja na kupeleka kwingine bila kuwawajibisha wahusika. Hata hivyo bima ya bure labda iishie kwa watoto tu. Watu wazima inapaswa wawajibike na afya zao.

Hakikaaa, ahsante

🙏🏾💪🏾
 
Back
Top Bottom