Kuyapa umuhimu mambo ya wengine hata kama kwako hayana umuhimu

LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
459
Reaction score
653
Wanadamu tunatofautiana fikra, vipaumbele nk, Hii ni kutokana na jamii iliyotuzunguka, changamoto tulizopitia, dini nk

Kuna jambo kwako linaweza lisiwe na umuhimu wowote na ukashindwa kuelewa kwanini mwenzako analipa thamani, usiwe mwepesi kumkatisha tamaa. Furahia naye hilo jambo kama ni la kheri na toa ushauri kwa njia nzuri ambayo haitomuumiza hisia zake au kumfanya ajione mjinga.

Mfano:

Mzazi kufanya graduation kubwa kwa mtoto wa Form 4. Kwa familia nyingi za mjini au waliozaliwa katika familia zenye wasomi wengi basi zitaona hii ni kutumia pesa vibaya.

Upo sahihi, lakini huenda kwenye familia ya huyu anayefanyiwa graduation yeye ndio wa kwanza kusoma mpaka form 4, kwahiyo kwao ni jambo kubwa kwasababu amekuwa lango la baraka katika hio familia. Kwahiyo furahia nao katika neema zao hata kama kwako sio neema kubwa.

Mfano 2:

Harusi kubwa, Kuna watu kuanzia wanakua wanawaza jinsi siku ya arusi yake itakavyo kuwa nzuri. Unaweza kuta katika akiba zake ana akiba special kwaajili ya siku ya sherehe yake tu. Ila wapo ambao wanafikra kuwa kile ni kitu cha siku moja, na cha kuangalia zaidi ni maisha baada ya ile siku ya harusi.

Wote wako sahihi, kwahiyo ambae anapenda sherehe kubwa msupport lakini kama mwanakamati ni vyema kumtengea asilimia kidogo kwaajili ya kuanzia maisha. Pia asiyependa sherehe basi ni kheri afanyiwe sherehe ndogo na kiasi kikubwa apewe kwaajili ya yale mambo ya kheri anayoyataka.

Mfano 3:

Mtu kufanya sherehe kubwa ya birthday ya mtoto wa mwaka 1, kwa mtazamo wa wengi ni kuwa anafanya show off, hio pesa angeenda kununua kiwanja nk

Ila huenda hio familia imehangaika kwa miaka kutafuta mtoto, kwahiyo watafanya lolote kwaajili ya furaha waliyo nayo, huenda ndoa ilikua inaelekea kuvunjika , hawana amani kwahiyo kwao ku gharamika kwaajili ya mtoto wao sio issue kwasababu ndio amewaletea amani iliyokuwa imepotea.

Point ni kwamba kila mtu ana kitu chake ambacho haki make sense kabisa na anaweza tumia gharama kubwa na usimuelewe, mradi ni cha kheri wewe muelewe na usimuhukumu kwasababu na wewe una kitu chako ambacho haki make sense.

Wapo ambao ni wapenzi wa viatu yani kwake kiatu hata kiwe laki 5 atanunua, ila huyo huyo hawezi msomesha mtoto wake shule ya million 5 na ana uwezo.

Yupo ambaye kwake elimu ni kipaumbele, yeye yuko radhi avae mitumba ila atampeleka mwanae shule ya million 7. Mwengine ugonjwa wake ni kula vizuri, yeye atanunua chakula hata cha 50,000 ila hawezi kupanda taxi au uber nk. Kwahiyo tusiwe wepesi kuhukumu, tujifunze vitu ambavyo ni muhimu kwa watu wetu wa karibu.
 
Nakuunga mkono, mimi nimeweka godoro chini sakafuni sijanunua kitanda, lakini ninapenda Multi Media, nina muziki mkubwa na TV nzuri kali. Nafurahia sana maisha.
 
Nakuunga mkono, mimi nimeweka godoro chini sakafuni sijanunua kitanda, lakini ninapenda Multi Media, nina muziki mkubwa na TV nzuri kali. Nafurahia sana maisha.
HAHAAA Hongera mkuu
 
Hakika umenena vyema.
Niseme tu Jamani ..nikibarikiwa kuongeza dunia mtoto wangu akifikisha mwaka tu li-birthday litamuhusu...😂
 
Show off tu, kwa sie wapenda gambe hizo zote ni upuuzi mbele ya gambe.

Niache bia nifanye birthday party kwani mi ni mwanamke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…