Kuyunga wa Baba Kiki na Bin Zubeiry darasa 1

Anselm

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2010
Posts
1,710
Reaction score
291
Pamoja na kuwahi kuishi katika nchi ya tofauti na Tanzania,ninaamini nchi yetu hii ni moja kati ya nchi zinazoongoza kwa kutofuatwa kwa maadili ya utendaji kazi hususani katika tasnia ya uandishi wa habari.

Kama ni kitu kinachovunwa kutoka darasani basi nina wiwa kusema kuwa Mwandishi Moh'd Kuyunga na "Kanjanja" Bin Zubeiry walihitimu darasa 1 na ndo maana siku zote wamekuwa wakishindwa kabisa kuficha mapenzi kwa team wanazozishabikia katika kazi zao za uandishi wa habari.

Tukiweka ushabiki pembeni kuna hoja ya msingi sana katika mada iliyowekwa hapa na Baba Kiki kuhusiana na habari ya kubezwa kwa ushindi wa Simba katika Kombe la Mapinduzi na habari nzima inaonyesha waziwazi jinsi Bwana Mohamed Kuyunga alivyo mnazi wa upande mmoja kama ilivyo kwa mwenzake "Kanjanja" Bin Zubeiry na habari yake ya tuzo za Wachezaji waliofanya vizuri katika mashindano hayohayo ya Mapinduzi Cup.

Katika habari hiyo kwa kushindwa kuzuia Mahaba yake kwa Mnyama "Kanjanja" alijikuta akipotosha wasomaji wa Blog yake kwa kuandika kuwa Peter Manyika, Hajibu na Ndemla wamechukua tuzo za Kipa bora, Mfungaji bora na Mchezaji bora wa mashindano.

Jamani hatukatai kila mtu ana uhuru wa kushabikia team aipendayo lkn ndo kwa kiwango cha kuandika habari ya uongo just kufurahisha nafsi yako bila kujali kama inapotosha Jamii.

cha kusikitisha zaidi inaonekana Kanjanja yuko shallow kwenye hiyo sekta anayoiandikia habari kwani hutokea mara chache sana kwa team moja kutwaa tuzo zote zinazohusiana na mashindano iliyokuwa inashiriki kama alivyotunuku yeye tuzo zote kwa wachezaji wa team aipendayo tena kwa kivuli cha Jopo la Waandaaji ni afadhali angeziita tuzo za "Bin Zubeiry" basi tungeelewa moja.

Alivyo na bahati mbaya sasa hakuna hata chaguzi 1 aliyoiandika yeye iliyotokea kuwa kweli kwani tuzo zote 3 zilikwenda kwa watu wengine kabisa. Kwa maoni yangu wote wawili Mbeza ushindi wa Simba na huyu mtunuku tuzo za magumashi wana kitu cha kukifanyia kazi katika kazi zao kama kweli wanataka kuzitendea haki kazi taaluma zao na pamoja na yote (haya ya kutobeza ubingwa wa Simba wa Mapinduzi Cup) hakuondoi dhana kuwa hii team ya Simba siku hizi imekuwa ni team ya makombe ya Mbuzi na yale ya Mabonanza.
 
Inajulikana wazi kwamba M.bin.Zubeiry sio Simba. Ni kanjanja tu asie kuwa na msimamo. Mara ya mwisho alikuwa Yanga na alifuatana na Yanga ilipochukua ubingwa wa Afrika Mashariki huko Uganda 1993.
 
Anselm, mbona Mahmud Zubeiry "Bin Zubeiry" ni mwanachama wa Yanga. Pia nilisoma habari yake iliyowataja Ajibu, Manyika na Ndemla. Mbona hakusema kama wao ndo watakuwa mfungaji bora, kipa bora na mchezaji bora wa mashindano isipokuwa alisema kuna uwezekano Ajibu (3 goals) akawa mfungaji bora kwa kuwa anayeongoza kwa ufungaji Msuva (4 goals) team yake imeshatolewa mashindanoni hivyo kama Ajibu atafanikiwa kufunga magoli mawili au zaidi katika mechi ya fainali anaweza kuibuka kuwa mfungaji bora. Simon Msuva aliibuka mfungaji bora.

Kuhusu Manyika alisema pia kuna uwezekano akawa kipa bora wa mashindano kwa kuwa alikuwa amefungwa goli moja tu hadi kuelekea mechi ya fainali lakini pia kuna uwezekano mkubwa Said Mohamed nae akaibuka kipa bora kwa kuwa nae alikuwa amefungwa goli moja (hapa hakuwa sahihi, Said alikuwa ameshafungwa 2 goals, mechi ya Mtibwa robo fainali NA JKU mechi ya makundi). Said Mohamed alitangazwa kipa bora wa mashindano.

Kuhusu Ndemla alisema kuwa kuna uwezekano kiungo huyo akaibuka kuwa mchezaji bora wa mashindano kama atacheza vizuri mechi ya fainali lakini pia kuna uwezekano mkubwa nafasi hiyo ikachukuliwa na beki Salim Mbonde wa Mtibwa Sugar ambae nae alikuwa amecheza vizuri sana hadi kuelekea mechi hiyo ya fainali. Beki Salim Mbonde aliibuka kuwa mchezaji bora wa mashindano.

Kwa maelezo hayo sikuona ubaya wa habari hiyo ya Bin Zubeiry, kama ni ukanjanja basi ahukumiwe kwa habari nyingine alizowahi kuziandika lakini si hiyo. Anayeweza kutuletea habari ile kama ilivyo hapa jukwaani bila kui-edit na afanye hivyo ili wadau ambao hawakuisoma waisome.
 
Masikrodinga uko sawa kabisa lkn hizo "kuna uwezekano" zote ku'base kwa Wachezaji wa team ya Simba(In 1st priority) peke yake ni dalili tosha ya kuonyesha mapenzi yake yamelalia upande gani,hlf Watu hamumjui huyu mtu,huyu mtu ni moja kati ya watu wanaoishi kwa mipango sana hapo Mjini kwahiyo sitashangaa kusikia kuwa ni Mwanachama wa Yanga au aliandamana na Yanga kwenda sehemu,lkn ukimfatilia kwa makini utagundua bayana ni shabiki wa upande wa 2 tena mkubwa kiasi cha kushindwa kuficha hilo jambo.
 
Last edited by a moderator:

Naunga mkono hoja. Na kwa kweli tatizo sio kuwa shabiki ila kuchanganya kazi na ushabiki kiasi cha kupotosha umma kwa maslahi ama ya unazi au tumbo au vyote
 
Back
Top Bottom