Habari zenu humu ndani. Naomba msaada wa kueleweshwa, mama mjamzito aliyeshauriwa kuzaa kwa operation kwa sababu mtoto hajageuka atapaswa kusubiri wiki ya 40? Au itabidi apasuliwe kabla ya wiki ya 36?

Mtoto ambae hajageuka, unaamanisha ametanguliza makalio au miguu(Breech). Ukilinganisha na aliyetanguliza kichwa, mtoto aliyetanguliza makalio ana uwezekano wa kupata matatizo zaidi wakati wa kuzaliwa, ingawa wapo pia wanaozaliwa bila tatizo lolote. Kwa wakinamama wajawazito wenye hali hii kwenye ujauzito wa kwanza(primegravida) au wale wenye kadirio la uzito wa mtoto zaidi ya kilo tatu(3kg) ni vizuri kufanyiwa upasuaji kabla uchungu haujaanza. Ili mtoto awe amekomaa vizuri mapafu na mifumo mingine muhimu ya mwili, upasuaji huu ufanyike angalau week ya 38 ya ujauzito.