Ishi vile utakavyo na si kama watu watakavyo.
Wana JF mimi mwenzenu nina mtoto mmoja tu,na huu ulikuwa ni mpango wa mimi na mke wangu kabla hata hatujaoana,mtoto wetu sasa ni mkubwa ana miaka 14,am not regreting for that and we are all quite happy,sasa kinachonishangaza mimi ni kuwa inakuwa kama kero,yaani nikutana na ndugu,marafiki,ninapokuwa kazini na hata watu wangine tu nisio na uhushiani nao wa karibu wamekuwa wakinilaumu mimi hata mke wangu "kwanini mmezaa mtoto mmoja tu si muongeze angalau mwingine",hili neno kwangu sasa naona ni kama kero kwangu,hebu nishaurini jamani hawa watu niwape majibu gani ili niwaridhishe.
Nadhani utaelewa tu siku moja kwanini wanakwambia hivo, yaweke haya maneno yangu.
Na bado kila siku zikienda atalia kupoteza wakati wake kuzaa katoto kamoja tu...Wengine wanataka kushindana kupanga maisha wakati Mungu ndo anawapangia.Haya maneno ya kizungu haya!!!!!! Sidanganyiki. Kama hujutii jambo hauhitaji vuvuzela kuwajulisha watu kuwa hujutii. Watu wataona tu kwa vitendo vyako. Nadhani wanaokuuliza wanahisi ama kwa maneno au vitendo vyako kuwa una regret kuwa na mtoto mmoja pekee.
Kosa kubwa sana kuzaa mtoto mmoja sababu hatakuwa na mtu wa kumsupport siku za mbele...Hakuna kitu kama damu.
Wacheni kuwainga wahindi na wazungu wale kule njaa zinawasumbua.
"Fazaa, if you have a good pension scheme and if you have prepared you retreat you won't need to be a burden for your kids in your old age.Kosa kubwa sana kuzaa mtoto mmoja sababu hatakuwa na mtu wa kumsupport siku za mbele...Hakuna kitu kama damu.
Wacheni kuwainga wahindi na wazungu wale kule njaa zinawasumbua.
Acha uchuro mkuu, ni uamuzi wa mtu/watu kuwa na idadi ya watoto kulingana na uwezo wa kutunza....sisi Waafrika/ Wabongo tunang'ang'ania kuwa na timu ya watoto matokeo yake ndio mara unakuta huyu katiwa mimba, kaka yake katia mimba mke wa mtu, mwingine sijui anavuta kitu ya Arusha halafu yule wa mwisho saa hizo yupo sijui Segerea.