Kuzikwa kwa ibada za dini tulizonazo au kuzikwa kipagani kuna manufaa gani kwa marehemu?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Mwezi uliopita, nilihudhuria mazishi ya rafiki yangu mmoja.

Kutokana na maisha yake aliyoishi hapa duniani, alikuwa haendi jumuiya, wala kutoa michango ya huko anakoabudia.

Umauti ulipomfika, kukawa na utata; kule kwenye dhehebu lake wakakataa kumzika, kwa sababu alikuwa haudhurii jumuia, wala kutoa michango.

Kilichofanyika, ni mtu alijitolea, akasoma somo katika biblia na marehemu akazikwa; ila hakukuwa na ibada yoyote.

Sasa nauliza, kuzikwa kwa ibada za dini tulizonazo, na kuzikwa kipagani; zina manufaa gani kwa marehemu?​
 
Mwezi uliopita, nilihudhuria mazishi ya rafiki yangu mmoja.

Kutokana na maisha yake aliyoishi hapa duniani, alikuwa haendi jumuiya, wala kutoa michango ya huko anakoabudia.

Umauti ulipomfika,kukawa na utata; kule kwenye dhehebu lake wakakataa kumzika, kwa sababu alikuwa haudhurii jumuia, wala kutoa michango.

Kilichofanyika, ni mtu alijitolea, akasoma somo katika biblia na marehemu akazikwa; ila hakukuwa na ibada yoyote.

Sasa nauliza, Kuzikwa kwa ibada za dini tulizonazo, na kuzikwa kipagani; zina manufaa gani kwa marehemu?​
Tafuta pesa
 
Kuna waliohifadhiwa bila kuzikwa kina Pharaoh lakini hawajafufuka mpaka leo.
Ukifa ndio basi tena haijalishi umezikwa, umechomwa moto au umetupwa kama mzoga, ni kwamba safari yako imefika ukomo. Kilichopo baada ya hapo hakuna anaejua.

Binadamu kwa kupenda kujipa umuhimu ndio tunaweka mazengwe mengi. Kwani wangemfanyia ada zote za mazishi wangepungukiwa nini ikizingatiwa kiimani mtoa hukumu ni Mungu. Wao kama kanisa wangetimiza wajibu wao, hukumu wamuachie Mungu.

Na ndio maana naupenda sana uislam, hata ukifia bar na iwe hujawahi kanyaga msikitini hata siku moja; ukifa na wewe ukijulikana ni muislam utazikwa na ada zote za mazishi zitafuatwa.
 
Ukishakufa umekufa mkuu

Kilichobaki unakua mzigo kwa uliowaacha, kususia kukuzika ni km kutoa funzo kwa wenye tabia km hizo

Kwa hio kwa marehemu yeye ameshaenda haimuhusu tena huo msala unakua wenu kwanin hamkua mnamkumbusha kuhusu kusali jumuiya na kutoa michango
 
Hakuna madhara yoyote. Lakini dini lazima iweke kitisho fulani kuwabana waumini, vinginevyo itaangamia. Zamani wakatoliki walikuwa wanauza kadi za wokovu. Na hata kama una ndugu yako alikufa siku nyingi ungeweza kumnunulia na huko aliko akaepuka adhabu. Tujiulize kama wakati ukristo unaanza , kwenye karne ya kwanza, je kulikuwa na ibada za kuombea waliokufa. au waliandaliwa tu na kuhifadhiwa.
 
Njia za kupiga pesa tu, kadi zilizotengenezwa viwandani ndio ziende kumfutia dhambi mtu aliyekufa kitambo , somatime hawa viongozi Wa dini hua wanatuona waumini Kama mapopoma aisee
 
Kuzikwa ni kuzikwa tu,hizi zingine ni mbwembwe tu ila Cha muhimu
Kama ulitenda mema utavuna pepo na kama ulitenda mabaya utachomwa moto iko wazi
 
Kwa sisi waislam ni kinyume mtu akifa jukumu la kuzika na kuistiri maiti lipo kwa sisi tulio hai. Kama kuna mtu kafa anatakiwa azikwe chap. Kama alikuwa mcha Mungu au Siye sio jukumu letu kuacha kumzika.
 
Ibada za mazishi na masomo husika ni kwa ajili ya waombolezaji walio hai. Marehemu anakuwa keshafunga vitabu vyake. Hakuna kinachoweza kusomwa kubadili namna alivyoishi au hatma ya aendako.
Kuna waumini wazuri lakini waliondoka kwa aina ya vifo visivyowezesha kuzikwa kwa heshima stahiki; mfano ajali za majini, milipuko au kuvamiwa na wanyama wakali na kuliwa bila kubakizwa.

Kutengwa na jumuiya ni kuonyesha namna gani Msamaha ulivyo mgumu hata kwa wanaotuhubiria Habari Njema. Nao ni binadamu tu. Hawana kauli ya mwisho katika hukumu ya haki.
 
Katika vitu ambavyo huwa nikitafakari nakosa majibu pia ni hili swala.hivi kiongoz wa imani husika usipo msomea misa marehemu na kumstiri ktk nyumba yake ya milele unapungukiwa nini?hili linanifikirisha ata kiongoz wa dhehebu husika kuna shida ktk fikra.hii kitu iliwahi kutokea Arusha mke imani tofaut na mumewe mauti ilipomkuta mume ktk imani yake waligoma kumzika kisa hashiriki mambo mengi ktk imani yake na michango alikuwa hatoi,lakini waupande wa imani ya mke wakaamua kuingilia kati wakamzika.nilijisikia vbaya sna kwani kati ya mungu na mwanadamu nani anayetakiwa ampe hela mwenzie,MUNGU amejitosheleza huu nimpango wa binadamu wachache kuvuna kwa manufaa yao tu.kwani tajiri haudhurii ibada wala mambo mengine ila michango anatoa atapewa misa siku akitoka duniani utasikia marehemu alikuwa anachanga sna.huu niutumwa wa fikra ndg zangu,tufanye lililo jema na mola anayoyataka ndg zangu dini haikupeleki popote bali imani yako na mola wako.shaloom
 
Mwezi uliopita, nilihudhuria mazishi ya rafiki yangu mmoja.

Kutokana na maisha yake aliyoishi hapa duniani, alikuwa haendi jumuiya, wala kutoa michango ya huko anakoabudia.

Umauti ulipomfika,kukawa na utata; kule kwenye dhehebu lake wakakataa kumzika, kwa sababu alikuwa haudhurii jumuia, wala kutoa michango.

Kilichofanyika, ni mtu alijitolea, akasoma somo katika biblia na marehemu akazikwa; ila hakukuwa na ibada yoyote.

Sasa nauliza, Kuzikwa kwa ibada za dini tulizonazo, na kuzikwa kipagani; zina manufaa gani kwa marehemu?​
Hili swali lako ni very subjective, umuhimu wake unategemea na personal importance au opinion ya tukio lenyewe kwa marehemu wakati akiwa hai.

Binadamu mwenyewe ndiye mwamuzi wa jambo kwendana na maono yake au uelewa wake.

Akiona hana umuhimu ataandika will au kuwaambia ndugu au watu wa karibu, nao watatekeleza kwendana na wosia wake, ndo maana wakati wa msiba kwenye vikao vingi utasikia, kwani marehemu alisemaje?
 
Katika vitu ambavyo huwa nikitafakari nakosa majibu pia ni hili swala.hivi kiongoz wa imani husika usipo msomea misa marehemu na kumstiri ktk nyumba yake ya milele unapungukiwa nini?hili linanifikirisha ata kiongoz wa dhehebu husika kuna shida ktk fikra.hii kitu iliwahi kutokea Arusha mke imani tofaut na mumewe mauti ilipomkuta mume ktk imani yake waligoma kumzika kisa hashiriki mambo mengi ktk imani yake na michango alikuwa hatoi,lakini waupande wa imani ya mke wakaamua kuingilia kati wakamzika.nilijisikia vbaya sna kwani kati ya mungu na mwanadamu nani anayetakiwa ampe hela mwenzie,MUNGU amejitosheleza huu nimpango wa binadamu wachache kuvuna kwa manufaa yao tu.kwani tajiri haudhurii ibada wala mambo mengine ila michango anatoa atapewa misa siku akitoka duniani utasikia marehemu alikuwa anachanga sna.huu niutumwa wa fikra ndg zangu,tufanye lililo jema na mola anayoyataka ndg zangu dini haikupeleki popote bali imani yako na mola wako.shaloom
Mkuu,
Paragraph na vituo ni muhimu sana.
 
Back
Top Bottom