Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Tafuta pesaMwezi uliopita, nilihudhuria mazishi ya rafiki yangu mmoja.
Kutokana na maisha yake aliyoishi hapa duniani, alikuwa haendi jumuiya, wala kutoa michango ya huko anakoabudia.
Umauti ulipomfika,kukawa na utata; kule kwenye dhehebu lake wakakataa kumzika, kwa sababu alikuwa haudhurii jumuia, wala kutoa michango.
Kilichofanyika, ni mtu alijitolea, akasoma somo katika biblia na marehemu akazikwa; ila hakukuwa na ibada yoyote.
Sasa nauliza, Kuzikwa kwa ibada za dini tulizonazo, na kuzikwa kipagani; zina manufaa gani kwa marehemu?
Asipishwe kwenye mateso ??Huwa nasoma vitabu vya wakatoriki, hawa jamaa wanaamini kuna sala ukiomba marehemu anaweza asipishwe kwenye mateso.
Njia za kupiga pesa tu, kadi zilizotengenezwa viwandani ndio ziende kumfutia dhambi mtu aliyekufa kitambo , somatime hawa viongozi Wa dini hua wanatuona waumini Kama mapopoma aiseeHakuna madhara yoyote. Lakini dini lazima iweke kitisho fulani kuwabana waumini, vinginevyo itaangamia. Zamani wakatoliki walikuwa wanauza kadi za wokovu. Na hata kama una ndugu yako alikufa siku nyingi ungeweza kumnunulia na huko aliko akaepuka adhabu. Tujiulize kama wakati ukristo unaanza , kwenye karne ya kwanza, je kulikuwa na ibada za kuombea waliokufa. au waliandaliwa tu na kuhifadhiwa.
Hili swali lako ni very subjective, umuhimu wake unategemea na personal importance au opinion ya tukio lenyewe kwa marehemu wakati akiwa hai.Mwezi uliopita, nilihudhuria mazishi ya rafiki yangu mmoja.
Kutokana na maisha yake aliyoishi hapa duniani, alikuwa haendi jumuiya, wala kutoa michango ya huko anakoabudia.
Umauti ulipomfika,kukawa na utata; kule kwenye dhehebu lake wakakataa kumzika, kwa sababu alikuwa haudhurii jumuia, wala kutoa michango.
Kilichofanyika, ni mtu alijitolea, akasoma somo katika biblia na marehemu akazikwa; ila hakukuwa na ibada yoyote.
Sasa nauliza, Kuzikwa kwa ibada za dini tulizonazo, na kuzikwa kipagani; zina manufaa gani kwa marehemu?
Mkuu,Katika vitu ambavyo huwa nikitafakari nakosa majibu pia ni hili swala.hivi kiongoz wa imani husika usipo msomea misa marehemu na kumstiri ktk nyumba yake ya milele unapungukiwa nini?hili linanifikirisha ata kiongoz wa dhehebu husika kuna shida ktk fikra.hii kitu iliwahi kutokea Arusha mke imani tofaut na mumewe mauti ilipomkuta mume ktk imani yake waligoma kumzika kisa hashiriki mambo mengi ktk imani yake na michango alikuwa hatoi,lakini waupande wa imani ya mke wakaamua kuingilia kati wakamzika.nilijisikia vbaya sna kwani kati ya mungu na mwanadamu nani anayetakiwa ampe hela mwenzie,MUNGU amejitosheleza huu nimpango wa binadamu wachache kuvuna kwa manufaa yao tu.kwani tajiri haudhurii ibada wala mambo mengine ila michango anatoa atapewa misa siku akitoka duniani utasikia marehemu alikuwa anachanga sna.huu niutumwa wa fikra ndg zangu,tufanye lililo jema na mola anayoyataka ndg zangu dini haikupeleki popote bali imani yako na mola wako.shaloom
P1Mkuu,
Paragraph na vituo ni muhimu sana.