Kuzindika gari

Alfredy1993

New Member
Joined
Sep 26, 2017
Posts
3
Reaction score
6
Samahani wanaJF mimi nataka kujua kama kuna haja yoyote ya kuzindika gari ukilinunua? Na je unaweza kuwa unapata ajali mara kwa mara kama hujafanya hvyoo kwenye gari lako?

Maana nasikiaga watu wanaongea ongea kuwa barabara ina malue lue mengi kwa hiyo unatakiwa kuzindika vyombo vya moto
 
Mungu hawezi kukusaidia kwenye ajali.

Angekuwa anasaidia kuepusha ajali basi kungekuwa hamna ajali.
Maana kila siku watu wanamuomba.
Mungu anakusaidia kwenye nini?
 
Mambo primitive kabisa
Gari jipya linaponunuliwa lazima lifanyiwe kafara.
Especially mabasi na malori ya masafa marefu..waarabu,wahindi na baadhi ya makabila .
Wengine wanafunga zindiko kama vitambaa au chochote kwenye matairi.
Au angalia mbele kwa dereva..

Si ajali zote za kimungu kuna zingine wanatengeneza binadamu.. kwa ajili ya kafara zao za biashara.


Sent from my M2101K7BG using JamiiForums mobile app
 
Vitambaa vinazuiaje ajali? Mambo mengine ni ujinga mwingi sana. Gari ni chombo cha kisayansi na suluhisho la matatizo yake lazima yawe ya kisayansi. Mfano mdogo tu, baada ya mabasi kuwekewa gadgets za ku- limit speed, ajali zimepungua sana. Hayo mambo ya zindiko ni upuuzi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…