Hoja ya mashabiki kuzomea timu ya Nyumbani ati ni sababu y'a timu zetu kukosa ushindi Nyumbani wala haina Mshiko, maandalizi y'a kipunguani au kimagumashi hawa ndiyo sababu tunapigwa tu kila mara. Kosa kubwa kuliko yote ni aina ya wachezaji tuliyokuwa nao kwenye vitabu vyetu, wengine hawafai Hata kucheza ndondo cup, hapa ninamaanisha viwango vyao viko Chini sana. Pili ni viongozi wa mpira tuliyokuwa nao, kuanzia vitabu, t. F. F hadi wa wizara husika, Wote hakuna Mwenye agenda endelevu kuhusu maendeleo ya soka, mara nyingi wanaangalia vile vitu walivyo n'a maslahi nayo, tena maslahi binafsi. Hadi usajili wachezaji viongozi husika uweka maslahi yao mbele kuliko klabu. Sasa ktk mazingira hayo unategemea Nini. Kocha kama mtaalamu apewe uhuru wa kufanya scouting y'a wachezaji. Kiufupi siasa za matumbo yetu ndiyo kikwazo ukubwa kwa mambo mengi y'a kutuletea maendeleo. Tunatoa maamuzi kwa kutanguliza matumbo yetu mbele. Kiufupi Sisi bado sana, si katoka soka tu, bali kwenye mambo mengi tu y'a msingi.