beibe nasty
JF-Expert Member
- Apr 11, 2012
- 1,640
- 524
Nimekerwa sana na kitendo cha naibu mkuu wa chuo cha CBE, Bw Othman Hemed na timu take kukataza wanafunzi kuvaa mitindo mbalimbali ya nguo na kuamuru wavae mitindo anayopenda yeye kwa kisingizio cha MAADILI YA KITANZANIA.
Kwanza nina uhakika (kama yupo anayebisha na aje), kuwa hakuna mwongozo wowote ni yapi MAADILI YA MTANZANIA. Kwa maana hiyo hayo maadili ya mtanzania ni kitu cha kufikirika tu, hakipo.
Watanzania tunaongozwa na katiba, na mwananchi yeyote ana haki ya kufanya lolote ili mradi asivunje sheria. Bw Othman aulizwe sheria gani anayokuwa amevunja mwanachuo akivaa jeans iwe ya kubana au kuachia? Bw Othman atuonyeshe katika sheria za nchi au za chuo ni wapi pameanishwa urefu wa sketi ili isiwe kimini, mitindo ya nywele au upana wa suruali. Tunafahamu sheria inakataza mtu mzima na mwenye akili timamu kuwa uchi hadharani, na imedefine uchi kuwa ni hali ya mtu kutokuvaa nguo zinazositiri uke/uume. Kuna nchi nyingine hairuhusiwi hata kuonyesha matiti nje, lakini kwa Tanzania haikatazwi, na ndio maana sio kitu cha ajabu kuwaona kina mama wakiwa vifua wazi.
Tunafahamu kuwa zipo tamaduni za makabila tofauti ya kitanzania, na kati ya hizo zipo za uvaaji zinazoruhusu sehemu kubwa ya mwili kuachwa wazi.
Kwa mantiki hiyo, kitendo cha uongozi wa CBE kuwazuia kusoma wanafunzi wanaovaa baadhi ya mitindo ya nguo na nywele, ambayo kwa uhakika wangu ni kuwa haivunji sheria za nchi, na wanaovaa ni watu wenye akili timamu na wanajua wanachokifanya, ni kitendo cha kizandiki, na kinafiki, na cha kipumbavu.
Akataze na kamkorogo aisee....
fafanua vema haki zipi za binadamu kakiuka na zimeanishwa ktk katiba ipi?
katiba haiheshimu tamaduni na haiba ya Mtanzania?
vaeni mavazi yanayostahili na msome acheni kuonyesha maungo nddio maana elimu ya sasa imeshuka sana
kinachokuuma ni nini, angekuwa dada yako anavaa vile ungefurah, kumbuka pale kuna watu wazima na heshima zao wanasoma, na ukifuatilia wale wanaovaa nguo za ajabu ni form4 wa division 4 na 5,
usishangae na sio cbe peke yake walianza saut sahiv mambo yapo shwarii watu washazoea kuvaa zao sket na gaun hhahahaha na inavoenda mpaka vyup vyote itakuwa hivoo chezea maadili wewe bt in other hand inasaidia kuwashape watu fulan fulan kuna watu wanavaa hovyo jamn hakuna mfano sasa na huko kuboost ziwa lataka lifike shingon uan akiinama linatoka