KERO Kuzuia benki kununua deni la bodi ya mikopo (HESLB) ilaumiwe bodi ya mikopo au or-utumishi?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mikopo ya kugharimia Elimu ya Juu imekuwa na mchango mkubwa sana kwa Taifa la Tanzania tangu kuanzishwa kwake. Ni ukweli usiopingika kuwa asilimia kubwa ya watanzania bado hawawezi kujigharimia elimu ya juu kwa vyanzo vyao wenyewe. Yamkini kusingekuwa na mikopo hii yawezekana tusingekuwa na idadi kubwa ya wasomi tuliyonayo sasa.

Pamoja na umuhimu wake kwa watanzania, Bodi ya Mikopo imekuwa ikikabiliana na changamoto ya mwitikio mdogo wa urejeshaji wa fedha kutoka kwa wanufaika wa mikopo hiyo.

Kwa upande mwengine jitihada za urejeshaji wa fedha hizo unafifishwa na Bodi pamoja na mamlaka nyingine za serikali kama vile OR-UTUMISHI kupitia utekelezaji wa mfumo wa ESS.

Kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa ESS, bank zilikuwa zinatoa huduma ya kununua deni la Bodi ya Mikopo kwa wanufaika ambao ni watumishi. Mfumo ule ulikuwa na manufaa kwa Bodi na watanzania kwa ujumla kwa sababu uliwezesha ukusanywaji wa fedha nyingi kwa mkupuo na hivyo kuzipeleka kwa waombaji wapya.

Kwa sasa huduma hiyo imesitishwa na upande wa serikali kwa sababu ambazo zinaonekana kuwa na udhaifu mkubwa. Banks zinasema hawaruhusiwi kufanya huduma za mikopo manually isipokuwa kupitia mfumo wa ESS. Na kwenye mfumo wa ESS huduma ya kuuza deni la Bodi haipatikani.

Swali langu ni kwanini huduma hii muhimu kwa pande zote; mlipaji na mlipwaji, imezuiliwa? Yaani hata kwenye kulilipa deni nako tunapangiwa? Hii haiko sawa na kunakatisha tamaa.

Nawasilisha!
 
Mfumo wa ESS ni kimeo kingine hicho kwa watumishi.Poleni sana.
 
Ess bado Ina madhaifu mengi sana,sioni dhamira ya uanzishwaji wake ikienda sambamba na matarajio ya kuanzishwa kwake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…