Christina samamba
Member
- Jul 22, 2022
- 20
- 38
Tatizo hili la kuzuia maiti ya mtu mara baada ya ndugu kushindwa kulipa pesa ni tatizo linalowatesa watu wengi sana hususan watu wenye kipato cha chini, Si kwamba watu wanafanya makusudi kutelekeza maiti za wapendwa wao hospitalini bali ni hali ngumu ya maisha na deni kuwa kubwa kuliko kipato chao.
Mfano kutoka kwenye chombo cha habari gazeti la Mwananchi la Alhamisi 23 septamba 2021 walichapisha kwamba hospitali ya Muhimbili ilishikilia mwili wa marehemu kwa jina Zena Musa mwenye miaka 30 baada ya ndugu zake kushindwa kulipa deni la shilingi milioni 1.6, ingawaje Serikali inajitahidi sana kukataza kitendo hiki mfano kutoka kwenye chanzo cha habari JamiiForums, Naibu Waziri wa Afya Dkt Ndugulile naye apiga marufuku kitendo hicho cha kuzuia maiti ambapo alisema "Ni marufuku hospitali kushikilia maiti kwa kile kinachotajwa hadi pale gharama za matibabu yake zitakapolipwa."
Hii ni baada ya mkasa kumpata bwana Shabani Mtepa mkazi wa Tandahimba baada ya kumpeleka mkewe kwaajili ya huduma kujifungua alifanyiwa upasuaji akajifungua mtoto mwenye afya njema lakini mama hakuwa na maendeleo mazuri ya kiafya kwami alivuja uchafu mwingi sana kwa muda wa siku nne mfululizo ilipofika siku ya tano alirudishwa theatre kwaajili ya upasuaji mwingine hali iliendelea kuwa tete kwani tatizo lile lile la kuvuja uchafu liliendelea na madaktari waliamua kumfanyia upasuaji kwa mara ya tatu hata hivyo hakukuwa na mafanikio yoyote kwa hiyo waliamua kumpa rufaa hospitali ya mkoa wa Mtwara (Ligula) kwa matibabu zaidi ila nao walishindwa kutatua tatizo lililomkabili mama huyo hivyo waliamua kumsafirisha hadi hospitali ya Taifa yaani Muhimbili.
Aliendelea kupata tiba hapo Muhimbili kwa siku nne na ilipofika siku ya tano yaani usiku wa kuamkia tarehe 7 Julai 2020 huyu mama aliaga dunia huku akimwachia mumewe mtoto mchanga wa wiki mbili na baada ya hapo ndipo kijana Shabani Shaban Mtepa alipoanza kufuatilia maiti ya mkewe ili akaihifadhi kwenye makazi ya milele lakini akakutana na kigingi cha kutakiwa alipe fedha milioni 1,470,800 huku akiwa na hali ngumu ya maisha.Hata kaburi lililoandaliwa kumpuzisha mwili wa marehemu ilibidi lifukiwe baada ya kuzuiliwa kwa mwili huo
Pia kutoka kwenye gazeti Mwananchi la Alhamisi tarehe 23 Septamba 2020 kuonesha kuwa tatizo ni kubwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alimwagiza Dkt. Gwajima kuangalia namna gani utaratibu maalumu utaandaliwa kuondoa kadhia ya maiti kuzuiliwa hospitalini "Tunaambiwa mtu asiende kuzikwa mpaka deni limelipwa lakini si deni la serikali nataka muweke mpango mnzuri wa kulipa deni bila kuzuia maiti "Moja kati ya mpango mzuri ni kushikilia gharama za matibabu wakati matibabu yakiendelea , sio siku mgonjwa amefarki dunia anaambiwa milioni 3 huku anafanya mpango wa namna gani atafanya taratibu za mazishi, Hii sio sawa naomba muweke mpangilio mnzuri wa kuyashughulikia haya aliagiza Rais Samia.
Pia kutoka kwenye chombo cha habari gazeti la Mwananchi la Ijumaa Septamba 6 2019 utaratibu wa kulipia gharama za matibabu kabla ya ndugu kuchukua maiti umehojiwa wabunge katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni ambapo mbunge wa viti maalumu Susan Lyimo alisema Serikali ina utaratibu wa kutoza gharama miili iliyohifadhiwa hospitalini jambo alilodai kusababisha simanzi kwa familia zisizokuwa na uwezo wa kulipa, lini Serikali itaacha kutoza gharama miili ya wanaofia hospitalini na kuhifadhiwa ili kupunguza simanzi kwa wafiwa "alisema Lyimo
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndungulile Kwa kulijibu swali Mheshimiwa Mbunge, alisema Miili ya wanaofia hospitali husika au kuletwa kutoka maeneo mbalimbali inatakiwa kuwekwa kwenye majokofu yenye ubaridi na wakati mwingine kuwekwa dawa za kusaidia isaharibike kwa mujibu wa sekta ya Afya yamwaka 2017 wananchi wanapaswa kuchangia gharama za afya ikiwa ni pamoja na matibabu na hata huduma za kuhifadhi wa maiti.
"Panapotokea changamoto za mwananchi kushindwa kumudu gharama za afya ikiwa na pamoja matibabu na hata huduma za uhifadhi wa maiti mwananchi huyo anapaswa kutoa taarifa kwenye uongozi wa hospitali husika ili kupata maelekezo ya namna ya kutatua changamoto hiyo amewahimiza wananchi kujiunga na bima afya kwa lengo la kupunguza gharama za matibabu toka mfukoni".
Ndiyo bima ya afya itasaidia kupunguza gharama za matibabu toka mfukoni ila si wote watakaoweza fanikiwa kuwa wanachama wa bima za afya hususan wenye kipato cha chini sana maana kiwango cha bima kipo juu kidogo mfano kwa watu wenye umri wa miaka 18 kiwango ni 192,000,384,000,516000,miaka 36 -50 kiwango ni 240,0000,440,000,612000 upande wa miaka 60 na kuendelea kiwango ni 360,000,660,000 na 984000
Licha ya makatazo yote hayo tatizo bado lipo na watu wanaendelea kuteseka
Inahitajika Serikali kuwaangalia suala hill kwa jicho pana zaidi kwa kusaidia kuandaa mikakati minzuri na sheria nzuri zitakazoziongoza taasisi hizi za afya katika utoaji wa huduma uliobora, Pia kunahitajika elimu ya kutosha kwa wanachi ili waweze kufahamu utaratibu uliowekwa na taasisi za afya baada yao kushindwa kulipa pesa ili kuchukua maiti ya wapendwa zao.
Wananchi wengi wamekuwa wakilalamika juu ya tatizo hili kwasababu pia ya kukosa elimu na uelewa kuwa inawezekana kwenda ustawi wa jamii na kupatiwa msaada ambao utawezesha hospitali kuwachia maiti kwa msamaha ila wananchi wengi hawalitambui hili.
Kwa hakika kunahitajika uboreshwaji wa sera za afya na sheria za afya kwa upana zaidi ili kuweza kuwafikia hata watu wasio na uwezo maana kwa Tanzania watu wanafikia 10% wanaotumia bima za afya baada ya kushindwa ada za wanachama ikibidi iangalie namna ya kuwasaidia watu wa hali hii ili kuweza kuondoa tatizo hili.

Upvote
10