Kimwakaleli
JF-Expert Member
- Apr 16, 2018
- 7,755
- 11,737
Habari Wana JF,Nimekaa na kutafakari nimeona nishee nanyi baadhi ya matukio ya kufanya kazi za kuajiriwa,iwe sekta Binafsi,mashirika au serikalini.
Kuna taasisi mahala Fulani kulikuwa na mkubwa mmoja, alikuwa na ndugu yake aliyekuwa anajishughulisha na biashara ya kuuza mchele wa jumla na Maharage kwa magunia kutoka kwa wakulima hadi kwenye masoko mbalimbali.
Sasa kutokana na kuona wafanyakazi kazi wakati mwingine Mambo hayaendi,akawaunga hao wafanyakazi na huyo ndugu yake,ili awe anawakopesha mchele au Maharage.
Wakati huko mchele ulikuwa unauzwa(100,000)laki Moja kwa gunia na Maharage (180,000)laki Moja na themanini, Mfanyakazi anakopa gunia Moja,mfano la mchele, Halafu analichukua badala ya kupeleka nyumbani kwenye familia, anaamua kupeleka dukani,na kuuza kwa shs(80,000)elfu themanini! Kumbuka atatakiwa amlipe huyu jamaa hela yake ya laki Moja(100,000).
Huu ni ubunifu au utumwa? Wale wa kusema maisha ya watu usiingilie wapitie kimya!
Ni hayo Wadau.