Wakuu nawasalimu.
Kuna ndugu yangu hapa Dar anahitaji mkopo wa sh 3m. nilivoongea nae hana dhamana ila ajira yake inaisha tar20 this november na anategemea kupata pensheni yake baada ya wiki mbili au tatu.
Anafikiria kulipa huo mkopo kwa pesa yake ya pensheni kwa riba ambayo mtaelewana na kuandikishiana kisheria mahala mtakapokubaliana.
Kama kuna mtu mdau humu amehamasika tunaweza kuwasiliana PM.
Asanteni kwa sasa
Mshauri huyo ndugu aende benki, ndo kazi zao, kukopesha na kudai.hapana shaka ushatapeliwa sana mpaka kila ishu unaona ni utapeli. ungewaza pia inawea isiwe utapeli
hahaa mkuu sio mimi ila kama uko willing naweza nikakupa contact zake PM
Wakuu nawasalimu.
Kuna ndugu yangu hapa Dar anahitaji mkopo wa sh 3m. nilivoongea nae hana dhamana ila ajira yake inaisha tar20 this november na anategemea kupata pensheni yake baada ya wiki mbili au tatu.
Anafikiria kulipa huo mkopo kwa pesa yake ya pensheni kwa riba ambayo mtaelewana na kuandikishiana kisheria mahala mtakapokubaliana.
Kama kuna mtu mdau humu amehamasika tunaweza kuwasiliana PM.
Asanteni kwa sasa
kiufupi anahitaji kwaajili ya ugonjwa kumsafirisha mzazi wake pamoja na gharama za matibabu. umeongelea kitu kuhusu mifuk hii kutoa fedha in advance nitamshauri afuatilie hilo. asante mkuuMshauri avumilie tu kwa sababu kupata fedha zake ni chini ya mwezi hiyo haraka aliyo nayo ni ya kitu gani? Kwanza amebakisha kama cku 10 contract iishe then 2 weeks apate hiyo fedha halali kwake bila kuipunguza kwa interest. Hata hivyo endapo ni issue ya shule, ugonjwa, biashara nk cku izi mifuko husika inatoa pesa inadvance, so bora awe mpole kuliko huu mchecheto alio nao wa kama moto wa mabua wakati muda umeisha.
umelipenda? sio gauni hio ni tshirt oversize
Mie naona hapa watu mnaremba sana.
Kwa ufupu Mleta mada ni Tapeli,au huyo mhusika anakuingiza kwenye Field ya Utapeli either kwa kujua au kutokujua.
-Yeye mpaka anastafu kesho kutwa hana hata Nyumba au Banda au hata shamba la kuweka dhamana tangu aajiriwe?
Maana mimi mjomba wangu alikuwa mlinzi pale NIT lakini alinunua hisa kiwanda cha Sigara kwa pesa zake hizo hizo za mawazo,na alijenga kwa kudunduliza.
-Alipoambiwa Bima ya Afya hakuilewa umuhim wake au?
-Anachuki gani na mwajiri wake hadi ashindwe kumfanyia utaratibu wa kukopeshwa ili akatwe kwenye pension yake
Hawa ndio waleee,wenye kukopa kazini kila wakimaliza deni hatimae inakuwa hawakipesheki,ila najua makazini kuna mifuko na misaada ya dharura kwa wazazi ambapo kwa namna yoyote ile utasaidiwa.
-Anaumwa nini na anasafirishwa kwenda wapi
-Anakopa 3m na yeye anakiasi gani
Ushauri:
Ukiwa kwenye ajira,jua kuna leo na kesho,Pombe na Madem hawana future kwenye maisha yako kijana.