Kanda kwa maji ya moto asubuhi na jioni ukiws umepakaa mafuta ya nazi tumboni ukilala jifunge kitenge au kanga nzito kuzunguka tumbo usikaze sana
we miezi mitano unaona mingi, kuwa na subira na punguza msosi litapungua, wenzako tangu wajifungue watoto wachaanza shule lakini tumbo liko palepale wala hawalamiki.imepita miezi mitano sasa tangu nilivyojifungua mtoto wangu wa kwanza, imetokea hali ambayo inanichukiza kwa kweli ni ili tumbo langu kuwa kubwa kama bado nina mimba, kwa ambaye anaweza kujua dawa yoyote ya asili ambayo inaweza kunisaidia kulipunguza, mazoezi yamenishinda nimejaribu sanaaa nashindwa kufwatilia, msaada please.
we miezi mitano unaona mingi, kuwa na subira na punguza msosi litapungua, wenzako tangu wajifungue watoto wachaanza shule lakini tumbo liko palepale wala hawalamiki.
wanawake wa kaskazini wanaona tumbo ni kuwa mambo mstari. utakuta mama anatumbo mzigo, anakula kitimoto alafu kando anashushia na ndovu bariiiidi, nyumbani ana ma house girl wawili mama mwenyewe kazi yake ni ya dukani, akikaa asubuhi kuamka jioni, kutwa nzima kutafuna tu.wao labda wanayapenda ndio maana hawalalamiki
1.Acha kunywa maji ya baridi kama ulikuwa unakunywa
2. Kula mlo mdogo mdogo(angalu mara sita kwa siku na si mara tatu kama wengi walivyozoea)
3. Kunywa kikombe kimoja au glass moa ya mai ya moto usiku kabla ya kwenda kulala
4. Epuka vyakula vya mafuta yanayoganda.
hapo kwenye kutokunywa maji ya baridi na joto hili ndo kasheshe!
Jenga tabia tu utazoea...hiyo ndio siri kubwa ya wachina na wajapani wengi kutokuwa na vitambi yaani kutokunywa maji ya baridi na ulaji bora wa chakula....wataalamu wanasema "you are what you eat"
Operation na huu ni mwezi wa 5 tu.! Hapana jaribu kufafanua kidogo maana ndani ya miezi sita hutakiwi kubeba hata ndoo ya 20lts.
Kanda kwa maji ya moto asubuhi na jioni ukiws umepakaa mafuta ya nazi tumboni ukilala jifunge kitenge au kanga nzito kuzunguka tumbo usikaze sana