Mosi,
Namba yako haikukamilika.
-Nina mashaka unamaanisha kuwa na biashara au vipi.
Kama hoja yako ni ya ukweli;
Kwanza, Unapaswa kuzungumzia madini yanayoitwa 'Zircon' Sio 'Silicon' kama ulivyotaja hapo juu.
Pili, Unao uhakika gani kuwa uliyonayo kweli ni Zircon?
Je, Unao utaalam au ufahamu
Wakutosha juu ya Mawe?
Nauliza hayo kwakuwa Mambo ya Mawe ni magumu na yanachanganya hata kwa walio wabobezi wenyewe watakuambia hivyo.
Mara nyingi huwa inatokea kudhania una aina fulani ya Jiwe kumbe sivyo kabisa.
Tatu, Kuhusu masoko ya mawe hayo na mengine,
Kifupi ni kuwa Kama unalo jiwe linalokidhi vigezo na viwango unauza kirahisi.
Ila yakupasa utulie, unaweza kupigwa pia.
Ufahamu wangu mdogo tu,
Kama uliyo nayo kweli ni Zircon,
Siwezi kukuhakikishia Bei ya sokoni kwakua,
Zircon zipo grade tatu tofautitofauti,
Rangi kama tisa tofautitofauti vilevile na hapo badochatujaangalia vigezo vingine muhimu vinavyoamua bei ya Jiwe sokoni.
Msaada mdogo ninaoweza kukupatia ni kusaidia kutambua
(si rasmi, kwa kuwa rasmi inahitaji utaalam unaogharimu fedha na katika mamlaka rasmi iliyopo kisheria)
Kwa kuanzia;
Naku-Pm namba yangu ya simu kwa mawasiliano zaidi,
Nifahamishe yafuatayo:
Hayo Mawe yako yana rangi gani?
Wastani wa jiwe moja ni gram ngapi?
Yametoka mkoa gani?
NOTE:
Namba ninayokutumia ipo WatsApp
Muhimu sana nitumie picha za hayo mawe.
Asante.