Kwa anayeifahamu mfumo wa elimu wa cambridge (tanzania)

sir echa

Member
Joined
May 28, 2010
Posts
85
Reaction score
3
Wadau naombeni msaada wa ufafanuzi kwa anayeelewa vizuri mfumo wa Elimu wa Cambridge unaotolewa hapa Tanzania.

Mimi nina mdogo wangu tulimpeleka kwenye shule moja (private) kwa ajili ya masomo ya sekondari mwaka jana. Wakati wanafunga mwaka, wakaambiwa wakifika kidato cha pili watachagua wanataka kusoma mfumo gani kati ya NECTA na CAMBRIDGE. Kwa kuwa hatu-ufahamu vizuri mfumo huo na faida zake nikashauri achague NECTA, mwaka huu kaingia kidato cha pili, alipofika shule waalimu wakamshawishi asome CAMBRIDGE na aachane na NECTA.

Tukapigiwa simu kupewa taarifa hizo kwamba mwaka huu hawana darasa la NECTA bali CAMBRIDGE tu, mpaka sasa tupo njia panda hatujui tumuache au tumuhamishe, kwani inaonekana shule hiyo haifuati mfumo wa NECTA, kwenye matokeo ya kidato cha 4 ya mwaka jana, shule hiyo haipo, ina maana wanafunzi wao walifanya CAMBRIDGE. Sasa nahitaji kujua faida na hasara za kumuacha dogo asome mfumo huo wa CAMBRIDGE mapema ili baadae isitokee kizaa zaa na kuanza kulaumiana wanafamilia.

Nawasilisha wadau naombeni ufafanuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…