Unataka kujua maana au unataka kufanya biashara? Kama unataka kufanya biashara ya corporate shares au corporate bonds wasiliana na Wakala wa Soko la Hisa (Dar es Salaam Stock Exchange) atakusaidia namna ya kuzipata.
Corporate shares = kwa maneno mengine ni Company Shares kama za TBL, CRDB, NMB, Twiga Cement, n.k.
Corporate Bonds = Ni Hati zinazotolewa na kampuni kwa watu au taasisi zinazoikopesha hiyo kampuni. Tofauti kubwa kati ya shares na bonds ni kuwa bonds zina muda ambao mkopaji anapaswa kurudisha huo mkopo kwa mkopeshaji (maturity period) wakati shares hazina muda. Ni utashi wa mwenye nazo kuziuza au kubaki nazo. Ni tofauti na Government Bonds ambazo zinauzwa (kukopa!) na serikali.