Kubemenda ni kile kitendo cha mwanamke mwenye mtoto mdogo ambaye bado anategemea kunyonya kushika mimba nyingine. Matokeo yake ni ya kwamba yule mtoto ananyonya maziwa pamoja na homoni za kulelea mimba, sasa zile homoni zinazorotesha ukuaji na afya ya mtoto kwa ujumla. Kwa hiyo, mtoto aliyebemendwa anadumaa na kuwa na afya dhaifu mno.