Kwa anayejua Sheria ya Mirathi, Urithi kwa watoto waliochangia mama, yupi mwenye haki?

rasha

Member
Joined
Sep 6, 2013
Posts
75
Reaction score
8
Huyu ni mtoto aliyekutwa na Baba kwa Mama.
Wakati huyu Baba anamuoa Mama,
alimkuta na watoto watatu (3) wote wa kike kila mmoja na Baba yake.
Na huyu Baba kipindi anamuoa Mama, alikuwa na Mtoto mmoja (1) wa kiume.

Wazazi hawa wakaona kwa ndoa ya kiislam, wakazaa watoto wawili (2)
Mmoja wa kiume na mwingine wa kike.

Wazazi hawa wakaachana na taraka ikatoka, wakagawana mali walizochuma pamoja, kikiwepo na kiwanja.

Baada ya kuachana, maisha yakaendelea,
Huyu Mama akapata Mume mwingine akazaa nae mtoto mmoja wa kiume. Lakini hawakufunga ndoa.
Kwa upande wa yule Baba akawa na mke mwingine pia nae hakufunga ndoa na anawatoto wengine.

Huyu mama kwenye ule uwanja wake alioupata kipindi wanaachana na mzazi mwenzie, akajenga nyumba na hii nyumba alijenga kabla hata hajakutana na huyu Baba mwingine. Akawa anaishi yeye na familia yake.

Kulingana na ugumu wa Maisha,
Aliona binti yake wa pili kwa kuzaliwa anahangaika kwa nyumba za kupanga,
Akamwambia ajenge nyumba hapohapo kwenye ule uwanja Ili binti yake asiteseke. Na akipata uwezo atafute eneo na kujenga.

Miaka michache baadae huyu Mama akafariki Dunia na kuacha watoto sita (6), watatu walikutwa na yule mtalaka wake, wawili walizaa na mtalaka wake, na mmoja baada ya kutalakiana.

Sasa basi yule binti aliyejenga kwenye uwanja anataka watoto wote (6) wakatiwe eneo Lao kutoka kwenye ule uwanja, na yeye pale alipojenga ndio kwake alipewa na mama yake. Na hakuna nyalaka zozote zinazozibitisha hilo.

Sasa Je,

(1) Kuna ulisi wa kwamama?

(2) Huyu binti anahaki yakudai ardhi anayoidai?

(3) Wale watoto wawili ambao Baba yao ndio alichuma na mama, haki yao iko wapi?

(3) Hawa watoto wengine nafasi yao inakuwa wapi katika hilo?

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu kwa mnayoijua sheria ya milasi.
 
Nadhani kinachoongelewa ni Mirathi na urithi
 
Wewe hata kiswahili hukijui? Milasi na ulisi ndio kitu gani?

Tiba
 
Kwa haraka, watoto wote wa yule Mama wanahaki ya kurithi mali alizoacha mama yao bila kujali baba yao ni nani. Wale watoto aliozaa na Bwana ambaye walipoachana waligawana mali, wanayo haki ya ziada ya kurithi mali kutoka kwa Baba yao.

Acha mawazo ya kizamani kwamba watoto wa kike hawana haki ya kurithi mali.

Hakuna aliyesema watoto wa kike hawana haki ya kurithi mali.
Hapo yeye anaposema ile sehemu aliyojenga ndio yake, ni sawa?
 
Wana haki ya kurithi kwa kufata sheria au mila gani?? Kwa kabila langu mtoto wa kike anarithi mali ya mme wake sio ya wazazi wake, na kwa dini yangu vivyo hivyo, lakini ustaarabu tu ndo unaotumika.. hata wakienda kwa kadhi, Kadhi atadecide in favour ya yule mtoto "Halali" wa kiume aliezaliwa ndani ya ndoa.
Hata wakienda kwa wazee wa makabila as long as ni patrillineal society huyo wa kiume atashinda... Ndo mfumo wetu Waafrika mtajaribu kumodify ila ndo ukweli
 
kuna njia tatu zinazoweza kuongoza katika kugawa urithi.
1. Will
2. kidini (Kiislam au kikristo)
3. kikabila
Njia zote hizi zinautofauti katika urithi.
Wewe umeongelea kikabila.
Sheria za sasa, kila mtoto ana haki ya kurithi.
Kwa upande wa hao watoto, kwanza mwenye mali ndiye aliyemruhusu kujenga, hiyo haina mjadala na pia yeye anapaswa kupata haki sawa na wenzake kwenye huo mgao wa mama yao.
 
mi kwa uwelewa wangu wa kisheria watoto wa mama wanahaki zte za kurth,na kwa kikristo pia wtoto waliochangia mama wanahaki endapo watahalalishwa watarth.Lakini ki islam mtoto wa nje aliechangia mama hana haki yyte ya kurth cz kwao mtoto wa nje ni haramu.Mfano; mm niwe na dada yngu ambaye 2mezalwa 2mbo m1 lakn baba tofaut bs m1atakosa.ila cz ya ubnadamu w2wengne huwafkria
 
Kwani kuambiwa kujenga ndio kupewa? Wewe kama Baba/Mama yako akikwambia mwanangu uwe unalima pale, ndio ushapewa chako mapema? Au uambiwe na mzazi usimamie mradi fulani kwahiyo ndio wako?
Ile ni fursa tu kama fursa nyingine na sio kama ushapewa chako mapema.
 
Sheria inasemaje hapo?
 
Hakuna aliyesema watoto wa kike hawana haki ya kurithi mali.
Hapo yeye anaposema ile sehemu aliyojenga ndio yake, ni sawa?

Ya kwake c kaambiwa na mama yake ajenge...tena uzuri kajenga mama akiwa hai..huo uwanja ni wa mama na watoto wote alowatoa tumboni mwake wana haki na huo uwanja cz ni wa MAMA yao...
 
Nyumba kweli ya kwake kwasabu yeye ndio kajenga, lakini kwenye uwanja wa familia.
Na kweli wote ni mamá yao, kwahyo mama aligawa urithi akiwa hai? Na watoto wengine akawaacha bila urithi.?
 
Kwani kuambiwa kujenga ndio kupewa? Wewe kama Baba/Mama yako akikwambia mwanangu uwe unalima pale, ndio ushapewa chako mapema? Au uambiwe na mzazi usimamie mradi fulani kwahiyo ndio wako?
Ile ni fursa tu kama fursa nyingine na sio kama ushapewa chako mapema.

so unashauri apokonywe? ninachomaanisha hasa ni kuwa hata mzazi wake ameonyesha thamani ya mtoto huyo kama watoto wengine, hapaswi kutolewa kwenye mirathi hata kidogo. Wanachopaswa kufanya ni kukaa chini na kugawana sawa kwa sawa ardhi ya mama yao.
 
Kwani kuambiwa kujenga ndio kupewa? Wewe kama Baba/Mama yako akikwambia mwanangu uwe unalima pale, ndio ushapewa chako mapema? Au uambiwe na mzazi usimamie mradi fulani kwahiyo ndio wako?
Ile ni fursa tu kama fursa nyingine na sio kama ushapewa chako mapema.
sasa hiyo nyumba utaipeleka wapi
 
Back
Top Bottom