mbagokizega
Senior Member
- Oct 22, 2016
- 111
- 297
Nipo hapa Kituo cha afya Kiburugwa na nina majibu ya vipimo mkononi, haki ya Mungu mke wangu kanidhalilisha.
Ni hivi, mke wangu ni mjamzito wa miezi 2 na mimba yake imekuwa ikisababisha tugombane Mara kwa Mara na hali hiyo ilinifanya nami ni react kwa kuamua kuchelewa kurudi nyumbani na kupunguza muda wa kukaa nyumbani na Mara nyingine kumletea za kuleta.
Basi juzi tulikuwa na mtafaruku mkubwa kiasi cha kufikia kutosemeshana ndani ya nyumba na ni kipindi hiko nilichokuwa najisikia kuumwa maumivu makali chini ya kitovu ndipo rafiki yangu anayefanya kazi hapa kituo cha afya akanishauri nipime mkojo pengine nna U.T.I.
Basi asubuhi ya Leo nimeamka mapema ili niende kupima na kwakuwa kituo hiki kinakuwa na foleni nikaamua kukojoa mkojo kidogo katika kikopo sasa wakati najiandaa kuvaa kumbe mke wangu alimwaga ule mkojo wangu na kuweka mkojo wake.
Jamaa aliyenipima hapa anasema vipimo vinaonesha nina mimba ya miezi miwili, tikarudia tena na tukamuita daktari wa kituo majibu ni hayohayo kwamba mi eti nina mimba ya miezi miwili, mi manesi na wahudumu wa hapa wananijua vizuri najua watanitangaza tu huko mtaani.
KWELI mimi wa kunidhalilisha hiviii? Mimi kweli nna mimba?
Aisee sikubali.