Kwa Bilioni hizi, naweza kujenga ghorofa ngapi?

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
Hello again, business guru's

Mchango kidogo wa mawazo, kujenga real estate, gorofa/ apartments kwa ajili ya renting/kupangisha kwa Kiswahili mnasema...

Je, budget ya bilioni zaidi ya moja na nusu[emoji385][emoji384][emoji387][emoji386] yaweza kutosha?? na kama ikitosha ni gorofa ngapi [emoji2515][emoji552][emoji539][emoji545] zaweza kukaa.

Nakaribisha wataalamu pia wa real estates na pia business guru's.
 
Mmmh ghorafa ya aina gani kama zipi toa mfano
 
Imaweza ikatosha...imaweza isitoshe....Factor ni location location location
 
kwa hiyo Billion 1.5 unapata ghorofa tatu kama zile Hostel za UDSM a.k.a Expansion joint

ila hadi uwe na connection na NHC
 
unaweza jenga lakini gharama hutegemea vitu vifuatavyo
location ya jengo lako
mchoro una structure za aina gani
Aina ya materials itakazotumia
Kandarasi

ni vema ukafafanua zaidi haya ili watu waweze kukuelewesha zaidi
 
Inategemea na aina za matirio utakazotumia.Mfano,atakayetumia nondo 18mm garama zake zitakuwa ni tofauti na aliyetumia nondo 12mm,uwiano wa simenti,mtaalamu/fundi wa ujenzi n.k
 
Una kiwanja reputed kwa ajili ya hiyo investment yako? Usije ukaenda kujengea nje ya mji ukategemea watu watakuja kupanga huko...kiwanja ndani ya mji kwa heka tatu andaa mil 400..kwaiyo toa mil 400 katika hesabu zako...zinazibakia ndo uzipigie mahesabu..
 
Wacheki TBA, Kumbuka gharama za jpm hostel. Wazee wa expansion jónt.
 
Sawa
 
Mwenye hizo pesa ni wewe [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hii ndio JF bhana.
 
Inategemea na aina za matirio utakazotumia.Mfano,atakayetumia nondo 18mm garama zake zitakuwa ni tofauti na aliyetumia nondo 12mm,uwiano wa simenti,mtaalamu/fundi wa ujenzi n.k
18mm ntatumia, but ndio ningetaka muongozo, hivi kuna contractor wazawa kweli ? Mana naona majengo mengi makubwa ni kampun moja ya kichina
 
unaweza jenga lakini gharama hutegemea vitu vifuatavyo
location ya jengo lako
mchoro una structure za aina gani
Aina ya materials itakazotumia
Kandarasi

ni vema ukafafanua zaidi haya ili watu waweze kukuelewesha zaidi
Location ya jengo ni katikati ya mji, mkuu unaonaje idea ya kumpa contract mkandarasi au kampun ya kikandarasi
 
18mm ntatumia, but ndio ningetaka muongozo, hivi kuna contractor wazawa kweli ? Mana naona majengo mengi makubwa ni kampun moja ya kichina
1.5b hio ni hela ya mboga na Co. itakayochukua hio tenda itakua ni co. Yenye class ya mwisho huko, kuna co. za wazawa wanajenga majengo ya bil. hata 100
 
18mm ntatumia, but ndio ningetaka muongozo, hivi kuna contractor wazawa kweli ? Mana naona majengo mengi makubwa ni kampun moja ya kichina
Wako wengi sana,na kama utawahitaji nitakusaidia kupata.Wapo wenye miradi mikubwa,midogo n.k na wote wako kazini wanapiga kazi kwa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…