Kwa Bilioni hizi, naweza kujenga ghorofa ngapi?

ha ha ha ha huwezi jua mkuu,watu wanavyanzo mbalimbali vya fedha mkuu
Hata siku moja mkuu nikufundishe kanuni ya maisha, kama mtu ananuka mavi usikae karibu yake nawe utanuka..nadhani umenisoma mkuu, basi baada ya hayo tutaendelea na yetu ya ukandarasi wa MAJENGO makubwa. Asante. Karibu pm.
 
Location ya jengo ni katikati ya mji, mkuu unaonaje idea ya kumpa contract mkandarasi au kampun ya kikandarasi
Kitu rahisi kwa hio hela nnachoona kwanza wewe tafuta uwanja wa kujenga (nadhani unao maana location umeshanipa) baada ya hapo tafuta kampuni ya ujenzi ambayo inajihusisha na designing pamoja na construction ukiipata ambayo ina jihusisha na designing ± construction ± consultant itakua vizuri ingawa consultant huwa inajitegemea ila mara nyingi huwa na kampuni za pembeni zinazojitegemea walizozianzisha ambazo zinajenga majengo wanayosimamia
Baada ya kuwapata hao, Watajie bajeti uliyonayo ya kujenga hilo jengo waambie wadesign jengo kulingana na bajeti yako huku ukiwapa mahitaji yako ya vitu ambavyo unataka viwepo katika jengo.
Lakini pia katika designing lazima uwafaamishe kuwa usimamizi na kazi zote za ujenzi ni wao ndio watahusika
Baada ya hapo unaingia nao mkataba kwa hio hela wajenge jengo ambalo mmekubaliana wewe utakabidhiwa jengo likiwa limekamilika kabisa.
Kuhusu malipo wakati wa ujenzi huwa unaweza lipa kwa awamu tofauti tofauti kila baada ya stage. Njia hii ni nzuri kwani inapunguza hujuma za materials fake katika ujenzi. Kwahio kila baada ya stage flani unatakiwa uwe na clerk of work anakagua unaidhinisha malipo
Clerk of work huyu ni engineer ambae utamuajiri binafsi hatohusika na kampuni yeyote inayohusika kwenye ujenzi yeye atakua anafanya kazi ya kukagua kama kampuni uliyoingia nayo mkataba inajenga kwa viwango
Hakikisha. Kama una fedha kiasi ambacho unahisi hakitatosha kwenye ujenzi unaingia mkataba wa kukabidhiwa jengo likiwa complete kwa maana kuna wakati gharama zinaweza kupanda au kushuka kwahio kama unahusika kwenye ujenzi lazima izo gharama zikuhusu na kupelekea kusimamisha ujenzi wakati mwingine sababu ya upungufu wa fedha
Lakini kampuni za ujenzi huwa wanajua kupambana na hayo mabadiliko ya gharama za ujenzi hivo ikiwa upande wao huwa ni rahisi ujenzi kuendelea huku gharama zikiwa zimebadilika na bado jengo likaisha vizuri bila usumbufu kwa client
 
Hivi kweeli mnaongelea mabilioni wakati mi mwenzenu nadaiwa kodi ya 150,000 ya miezi 6

Hapa nawaza naenda kusemaje kwa maza house,ila mlivyo na dharau Mnadiscuss billioni

Saweni Mungu yupo upande wangu,anaona huu unyanyasaji wenu.
 
Nakushukuru sana Smart Technician
 
Hiyo si ni hela ya mboga kama nikimnukuu vizuri Prof. Tibaijuka?
 
Kujua utaweza kujenga ghorofa ngapi inategemeana na vitu vifuatavyo:-

1. Ramani ya jengo - jengo lina ukubwa gani; Mara nyingi kuna rate ambazo ziko zinakuwa charged kwa square meter kwa standards tofauti. Lakini pia ramani ioneshe inaweza ku_accommodate watu wangapi


2. Materials - kwa sehemu kubwa uchaguzi wa materials ndio unatoa picha halisi ya gharama za jengo; maana ubora wa jengo inategemeana na materials zilizotumika, kwahiyo hili ni swala la kuzingatia


3. Site location - eneo ambalo jengo litajengwa kuna athiri bajeti ya mradi, kwa mfano maeneo ambayo upatikanaji wa materials ni gumu, basi kuna uwezekano mkubwa sana wa gharama kuongezeka, lakini pia hali ya site na kwa maana inahitaji maandalizi kiasi gani kabla ya kuanza ujenzi pia inaongeza gharama!


Ili kuwa na uhakika ni vizuri ukiwa na ramani tayari, itakuwa rahisi sana kupata ushauri ambao ni halisi!

Lakini kwa sasa ukiniuliza kulingana na uzoefu ninaweza kukwambia jengo la floor 3,2, au 1.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukrani, ila kwa hapa kwetu kuna kampun za ujenzi ambazo zina reputation nzuri ya kujenga majengo especially magorofa ?!
Sent using Unataka kujua ili iweje
 
Shukrani, ila kwa hapa kwetu kuna kampun za ujenzi ambazo zina reputation nzuri ya kujenga majengo especially magorofa ?!

Sent using Unataka kujua ili iweje
Kwenye field ya construction hiyo ni project ndogo sana! Kampuni ni nyingi sana, mpaka Class 6 inaruhusiwa kujengo hadi ghorofa 2.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe, project kubwa kwenye connstruction ya gorofa ni kuanzia gorofa ngapi

Sent using Unataka kujua ili iweje
Ukubwa wa project unapimwa kwa kuangalia gharama halisi za jengo! Lakini pia na complexity ya jengo kwa maana ya vifaa vinayohitajika katika kufanikisha ujenzi! Kingine ni construction methodology inayohitajika, ndio inatoa picha ya size ya project.

Binafsi naweza kusema, ghorofa 5 nakuendelea lakini kuna majengo mengine ni chini ya ghorofa 5 lakini yakawa makubwa kwa maana ya mita za mraba kwa kila ghorofa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…