Elections 2010 Kwa data hizi kikwete lazima ashinde kwa kishindo

Hacheni ubaguzi, janja yenu inajulikana mnamchoka MOD ili haifute hii hoja.


Kwa nini zinatolewa data za Manzese? Kwa nini mabadiliko ya elimu yaliyofanyika kwa jamii zilizopo pembezoni hasa za wawindaji na wafugaji yaani Wabarbaig, Wamasai na Wahadzabe. Ni asilimia 1 tu pengine ndio wanaobahitika kwenda shule. Tuzingatie usawa.

_______________________________________________
 
Waandishi wa Annur wanatakiwa kuelimishwa tofauti ya vyumba vya madarasa vilivyojengwa kwa mchanganyiko wa saruji hafifu na kitu kinchoitwa shule. Watoto ambao hata kuandika majina yao hawajui sidhani kama ni kitu cha kujivuni kuwapeleka Sekondari. "2010 HATUDANGANYIKI"
 
Al Hudda kuja na twakimu za maeneo ya DSM na kusema JK kafanya kazi kubwa katika nyanja ya Elimu ni kutumia takwimu vibaya sana. DSM ni sehemu ndogo ya nchi mzima kwa hiyo haiwezi ikawa kigezo cha mafanikio katika Tanzania nzima. Mimi ninakotoka katika Jimbo la langu la uchaguzi la Nkenge sijaona shule hata moja iliyojengwa tangu 2005 hadi leo. Hata moja. Juzi juzi tumeambiwa kwamba hata foleni DSM ni dalili ya maendeleo. Ni matusi!!
 
life cycle of malaria in progress: Malaria sugu a.k.a dubo,a.k.a antibiotiki,a.k.a vuvuzela na mengine mengi,yaani let me give u a simple tip,kwenye post zake mjibuni kama mgonjwa wa schizophrenia,majibu yote yawe tangential na post zake,nyie mkibishana naye anazidi kupata bichwa,nyie mjibuni mambo amabyo haya husu na post yake,atachoka mwenyewe.
 
Nenda shule ya msingi hekima pale buguruni,watoto wa darasa la 4 wanaojiandaa na mtihani wao wa taifa hawajui kusoma na kuandika,endeleeni kuishi kwa takwimu
 
Kikwete hongera kwa kufanikisha haya katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, wewe ndo chaguo letu, tutakupa kura uendelee na mapambano

Idadi ya wanafunzi wanaoendelea na na elimu ya sekondari imeongezeka

-Wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi na kuendelea na elimu ya sekondari wameongezeka kutoka wanafunzi 493,636 mwaka 2005 na kufikia wanafunzi 999,070 mwaka 2009.
-Kuongezeka kwa wanafunzi wanaogharamiwa na serikali kutoka katika familia zenye kipato duni na yatima , kutoka wanafunzi 16,345 na kufikia wanafunzi 58,843 mwaka 2009

Mafanikio ya elimu ya Juu ni pamoja na

-kuongezeka kwa udahili katika vyuo vikuu ambapo udahili wa wanafunzi umeongezeka kutoka wanafunzi 40,993 mwaka 2005 na kufikia wanafunzi 111,078 mwaka 2010.
-Idadi ya vyuo vikuu imeongezeka kutoka vyuo 23 mwaka 2005 hadi kufikia vyuo vikuu 31, 2010.
-Kuweza kujenga chuo kikuu cha Dodoma chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 40,000 kwa mwaka na kwa sasa kuna wanafunzi 17,282.
-Kumekuwepo na Ongezeko la utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu kutoka wanafunzi 42,729( sh. 62.5) mwaka 2005 na kufikia wanafunzi 58,841 ( Sh. 140 bilioni) mwaka 2009.
-Programu za vyuo vikuu zimepanuka na kuboreshwa ambapo vyuo vikuu vya Sokoine, Mzumbe na Dodoma vinatoa shahada ya Elimu.
 

Hujakosea mkuu! you are very very intellingent than any! Heheee! kwani angekuwa mkapa hata walimu angewashusha kutoka mbinguni. Yaelekea wewe hata maana ya MMEM huijui na iliendeshwaje hujui.
 

Hujakosea mkuu! you are very very intellingent than any! Heheee! kwani angekuwa mkapa hata walimu angewashusha kutoka mbinguni. Yaelekea wewe hata maana ya MMEM huijui na iliendeshwaje hujui. Ila unafikiria kurusha ngumi tu. sijui ungepigana na nani, na sijui kama unaziweza.
 
Mleta thread amesema annur na si alhudda. Yaelekea wewe haupo Tanzania ndo maana huoni hata shule moja katika kata yako. Bila shaka hakuna hata mwana JF yeyote atakaekubaliana nawe kwa hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…