Kwa dhati kabisa tuwakumbuke wafuatao kwenye sala na dua zetu

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Tuwaombee;

1. Watu wote wanaopambana na magonjwa mbalimbali au majeraha ya ajali. Mungu awape nafuu na warudi kwenye hali zao kawaida.

2. Watu wote wanaohudumia wagonjwa. Wasikate tamaa na waweze kumudu gharama za matibabu ya wapendwa wao.

3. Watu wote wanaopambana na madeni. Mungu awatie moyo na kuweza kulipa madeni yao. Pia waweze kueleweka na wadaiwa wao.

4. Wote wenye matatizo kwenye ndoa zao. Waweze kufikia maelewano na wenza wao na kurudi kwenye furaha na amani.

5. Wenye vipato duni visivyotosheleza mahitaji yao ya lazima kama binadamu yaani chakula, malazi na mavazi. Mungu awainue hawa.

6. Vijana wadogo waliohitimu vyuo ila wanasota mtaani bila ajira hata ya kujitolea. Hawa wanahitaji kushikwa mkono.

AMEN
 
Thread kama hii kwakua Mzabzab,extrovert,mshana Jr na Faiza fox. Hawachangii basi tegemea kuona inaishia comment 20.
 
Tuwaombee;

1. Watu wote wanaopambana na magonjwa mbalimbali au majeraha ya ajali. Mungu awape nafuu na warudi kwenye hali zao kawaida.

2. Watu wote wanaohudumia wagonjwa. Wasikate tamaa na waweze kumudu gharama za matibabu ya wapendwa wao.

3. Watu wote wanaopambana na madeni. Mungu awatie moyo na kuweza kulipa madeni yao. Pia waweze kueleweka na wadaiwa wao.

4. Wote wenye matatizo kwenye ndoa zao. Waweze kufikia maelewano na wenza wao na kurudi kwenye furaha na amani.

5. Wenye vipato duni visivyotosheleza mahitaji yao ya lazima kama binadamu yaani chakula, malazi na mavazi. Mungu awainue hawa.

AMEN
Amen ,amen, amen!
una akili sana, hatuombei marehemu, roho ikishatoka ni kusubiri hukumu, tunaombea walipo.
Hii tabia ya wanasiasa kusema tunaombea marehemu alale mahali pema peponi ndi inawafanya wawe mafisadi ili wakifa wafanyiwe sala kwa fedha walizoiba.
 
Back
Top Bottom