Nilikutana na engineer aliyegraduate Iran, anafanya kazi Perth, yeye anasema alifanya applications zote akiwa Iran, baada ya kupata visa alitumia agent kupata kazi na hakuhamia australia mpaka alipopata kazi, . Ilimchukua muda kupata visa (processing time ni miezi 7 ) na agent alimtoza hela nyingi lakini alimudu kumlipa kwa sababu kazi aliyopata inalipa vizuri.
Iwapo kazi yenyewe ina faida za maana (ujuzi, kipato etc), na kuna uwezekano wa kupata hiyo visa hata kazi mtu akiwa TZ basi inaweza ikawa option kwa wale wenye interest. Nakubali kabisa kwamba haina maana yoyote mtu kuacha kazi yake ya uinjinia Bongo (hata kama haimpi faida inayomridhisha) kwenda kumanga manga na mabox kwenye nchi za watu.