Kwa fani ya umeme, utawezaje kufanya biashara?

Agustini john

Member
Joined
Aug 9, 2014
Posts
29
Reaction score
3
Kama ukisomea mambo ya umeme utawezaje kufanya biashara? Na kama ukifanya biashara utaweza kufanikiwa? Naombeni mawazo yenu.
 
Ndugu, swali lako ni la ajabu sana lakini naomba nikujibu kama ifuatavyo;
Kwanza biashara haijalishi fani uliyosoma.

Kuna hata ambao hawajasoma fani yoyote lakini wanafanya biashara. Hivyo ukisoma fani ya umeme waweza kufanya biashara yoyote ile. Pia waweza kutumia ujuzi wako kujiari katika kazi za umeme kama kufanya wiring kwenye nyumba n.k.

Pili unapofanya biashara unanufaika na faida. Unapofanya biashara unaanza na mtaji. Inategemewa kwamba utapata faida. Utatumia sehemu ya faida kukuza mtaji na sehemu nyingine kuweka akiba na sehemu nyingine kutumia katika kujikimu kinaisha. Hivyo utakuwa umenufaika.
 
,ie nakuomba uone kama vile taaluma uliyosomea ni duka, sasa kitu cha msingi ni je unauza bidhaaa gani dukani mwako, je wateja wanazo taarifs wa upatikanaji wa bidhaa wanazohitaji kuwa zinapatikana dukani mwako?????
Yaani ukikaa na kuandika majibu ya hayo maswali bizuri haitakuchua mida mirefy na utaona mabadiliko na kipato kuzidi kuongezeka( how I wish all wanachukuo wangelijua hili na kuandika thesist/consept not basing on those two question tugeona mabadiliko ya hali ya juu Tanganyika / Tanzania na kusigekuwa,na ukosefu wa ajira)
 
Ni kweli, wa TZ tuuze fani zetu. Ila tufanye kazi serious tuache porojo.
 
Fungua duka lenye vitu vya umeme kama cables, vifaa vya umeme wa ndani, taa za nje na ndani, alarm systems na vinginevyo vyenye mahitaji ya installation kwenye nyumba.

Wateja wakija wape na business card kwamba unaweza fanya installation ya umeme kwenye nyuma mpya, wakitaka vitu walivyonunua kwako unaweza wafungia kwa charge nafuu, pia unaweza waweka salama zaidi kwa kukagua kazi za umeme zilizokamilika kuhakikisha zimefanyika kiusalama, toa ushauri wa bidhaa bora zilizopo dukani kwako na faida za kuwa kwenye nyumba za watej.

Ukiona watu wanajenga wape business card ya bidhaa zako na vitu vya umeme unavyouza na service unayoweza toa ikifika muda wa kufanya installation kama wakikuitaji unaweza kwenda.

Just get creative, before you know utajikuta una warehouse ya bidhaa na biashara kubwa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…