Kwa hali hii CCM hatuwezi kujipiga kifua

Kwa hali hii CCM hatuwezi kujipiga kifua

Wimbo

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2012
Posts
866
Reaction score
625
Tunaposifia kuupiga mwingi tujihoji kabla ya November 2024 na 0ctober 2025, miradi mkakati hasa ya miunddombinu ambayo kukamilika kwake kungechechemua uchumi wa Nchi imesimama, wakandalasi hawajalipwa pesa, kwanza hili ni janga kwa sababu tunaongeza riba lakini ni angalizo la uimara wetu na usimamizi wetu wa mapato usioakisi ukubwa wetu, kama tumekopa fedha nyingi zimefanya nini?

Hata kama zimefanya vitu je zimeelekezwa kwenye vipaumbele. uko ujenzi wa barabara mf. Barabara ya Itoni -lusitu Njombe imesimama mpaka mkandalasi sasa hivi anahamisha vifaa kwenye miradi mingine endapo nvua itaanza ambayo si muda mrefu njia itajifunga. uchumi kwa wana Manda, Ludewa njombe utaathirika, hili tunalitazamaje?

Ningekuwa mimi kiongozi wa Nchi nisingeangalia masuala ya kuwapeleka wasanii Korea , kulipa magoli ya mama, kununua magali mapya ya wakuu wa wilaya n.k. ningeelekeza kidogo kilichopo kwenye vipaumbele zalishi.

watanzaniani waelewa tena wavumilivu mf. Mama angetokea akawaomba watanzania tuahilishe uchaguzi wa serikali za mitaa hadi mwakani ili tufanye pamoja na uchaguzi mkuu kupunguza gharama tungemuelewa na hizo kiasi cha takribani Bil. 800 zitakazotumika huku na mwakani tukitegemea kutumia kiasi zaidi hicho zitumike kumalizia au kupunguza ukata kwenye ujenzi wa miundombinu ingependeza, kuimalisha reli ya uhuru ili kupunguza uharibifu wa barabara inayobeba zaidi ya maloli mia tano kwa siku kuvuka mpaka wa Tunduma tungemuelewa zaidi.

Mama Samia unafanya vizuri lakini nina wasiwasi na wanaokushauri ktk maamuzi unayoyafanya. Mungu akusaidie kuna sifa nyingi wanazokupa na kinafiki na zenye hira ndani yake (kwa mtazamo wangu) wanisamehe tu kama watajisikia vibaya.
 
Vitabu vya dini vyote vinasema mwanamke ni mlezi wa familia sio mtawala,ccm sasa hivi hawana hamu mana uchumi unaliwa na familia na watu wake wa karibu. Mpka 2025 utaona timuatimua huko chamani ikipamba moto.
 
Back
Top Bottom